ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 3, 2019

MIKOA MINNE YA TANZANIA KUPULIZIWA DAWA YA KUUA MBU WA DENGUE

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati akiwa na viongozi wenine akiwemo Naibu Waziri wa wizara hiyo, Dk. Faustine Ndugulile wakati alipotembelea eneo la jangwani jijini hapa.

Mikoa ya Dar es Salaam na Tanga imetakiwa kushirikiana na wananchi kuangamiza mazalia yote  ya mbu kwa kunyunyizia dawa za kuua mbu wapevu kwa kutumia mashine kubwa.

Hayo yamesemwa mapema Juni 2.2019 na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati alipotembelea eneo la jangwani jijini hapa.

Waziri Ummy amefanya maamuzi haya baada ya mikoa hiyo kuathiriwa na ugonjwa wa homa ya Dengue"nimeelezwa mkoa wa Dar es Salaam unahitaji kununua lita 1000 za dawa aina ya Acteric 500 na Icteric 300 kwa ajili ya kunyunyizia mbu wapevu katika mitaa,ninawataka wakurugenzi wa Manispaa kuhakikisha dawahizi zinanunuliwa mara moja na.kufanya upuliziaji katika maeneo yenye mbu"Alisisitiza Wazirj Ummy.

Aidha, amewataka wamiliki na waendeshaji wa migahawa,bar,mahotel,saluni,gareji,mashule,maofisini na sehemu zote zinazozunguka maeneo yao wanakagua mazalia ya mbu,kufukia madimbwi ya maji na kufanya usafi kwa ajili ya kuangamiza mazalia ya mbu.

Hata hivyo alivitaka vituo vya kutoa huduma za afya vikiwemo vya watu binafsi kuzingatia taratibu na miongozo iliyopo ya kutoa taarifa kwa uongozi wa afya wa halmashauri kila siku wanapopima na.kugundua kuwa ntu ana ugonjwa wa dengue bila kuacha.

Wakati huohuo Naibu Waziri Dkt.Faustine Ndugulile amewataka watoa huduma za afya ambao sio waaminifu kutotoa majibu yasiyo sahii ya dengue na kutoa dawa zisizostahili kwa ugonjwa huu

"Tutaanza kuchukua hatuakali kwa watu wanaojirekodi na kusambaza klipu zinazosema watu wanywe maji ya mipapai au kupaka mafuta ya nazi ,tunasema ugonjwa huu hauna tiba hivyo mtu yeyote anayeona ana dalili hizo ni kufika kituo cha afya "Alisema Dkt.Ndugulile

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam  Abubakari Kunenge amesema kama mkoa  watatekelza maagizo yote na kuteketeza ugonjwa huo hivyo kuhakikisha wanaanza kupuliza dawa kwenye maeneo ya mazalia na kutoa wito kwa wananchi kushirikiana kufanya usafi wa mazingira na kuondoa mazalia ya mbu kwa ustawi wa afya
Na.WAMJW,Dar es Salaam

Mikoa ya Dar es Salaam na Tanga imetakiwa kushirikiana na wananchi kuangamiza mazalia yote  ya mbu kwa kunyunyizia dawa za kuua mbu wapevu kwa kutumia mashine kubwa.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati alipotembelea eneo la jangwani jijini hapa.

Waziri Ummy amefanya maamuzi haya baada ya mikoa hiyo kuathiriwa na ugonjwa wa homa ya Dengue"nimeelezwa mkoa wa Dar es Salaam unahitaji kununua lita 1000 za dawa aina ya Acteric 500 na Icteric 300 kwa ajili ya kunyunyizia mbu wapevu katika mitaa,ninawataka wakurugenzi wa Manispaa kuhakikisha dawahizi zinanunuliwa mara moja na.kufanya upuliziaji katika maeneo yenye mbu"Alisisitiza Wazirj Ummy.

Aidha, amewataka wamiliki na waendeshaji wa migahawa,bar,mahotel,saluni,gareji,mashule,maofisini na sehemu zote zinazozunguka maeneo yao wanakagua mazalia ya mbu,kufukia madimbwi ya maji na kufanya usafi kwa ajili ya kuangamiza mazalia ya mbu.

Hata hivyo alivitaka vituo vya kutoa huduma za afya vikiwemo vya watu binafsi kuzingatia taratibu na miongozo iliyopo ya kutoa taarifa kwa uongozi wa afya wa halmashauri kila siku wanapopima na.kugundua kuwa ntu ana ugonjwa wa dengue bila kuacha.

Wakati huohuo Naibu Waziri Dkt.Faustine Ndugulile amewataka watoa huduma za afya ambao sio waaminifu kutotoa majibu yasiyo sahii ya dengue na kutoa dawa zisizostahili kwa ugonjwa huu

"Tutaanza kuchukua hatuakali kwa watu wanaojirekodi na kusambaza klipu zinazosema watu wanywe maji ya mipapai au kupaka mafuta ya nazi ,tunasema ugonjwa huu hauna tiba hivyo mtu yeyote anayeona ana dalili hizo ni kufika kituo cha afya "Alisema Dkt.Ndugulile

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam  Abubakari Kunenge amesema kama mkoa  watatekelza maagizo yote na kuteketeza ugonjwa huo hivyo kuhakikisha wanaanza kupuliza dawa kwenye maeneo ya mazalia na kutoa wito kwa wananchi kushirikiana kufanya usafi wa mazingira na kuondoa mazalia ya mbu kwa ustawi wa afya.

Na.WAMJW ,Dar es Salaam

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakiangalia moja ya maji machafu kwenye eneo hilo la Jangwani ambayo pia ni moja ya mazalia ya mbu wa Dengue ambao wameelezwa kuzaliana maeneo hayo. Wengine ni  viongozi wskiwemo Naibu Waziri wa wizara hiyo, Dk. Faustine Ndugulile, Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam na Mganga Mkuu wa Wizara ya Afya 
 
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  akitoa maagizo kwa Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam (RAS) Aboubakary Kunenge  juu ya hatua za haraka za kuhakikisha dawa zinapulizwa kwenye maeneo yote yenye viashiria vya mazalia ya mbu. Kuilia ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Dk. Faustine Ndugulile wakati alipotembelea eneo la jangwani jijini hapa.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua eneo hilo la Jangwani kampeni ya kutokomeza uchafu ikiwemo sualala mazalia ya mbu wa Dengue. 
PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE, DAR ES SALAAM, TANZANIA.

No comments: