Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias John Kwandikwa (kulia), akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Morogoro Mhandisi Godwin Andalwisye (kushoto), kuhusu mradi wa ujenzi wa daraja la mfuto (drift) katika mto Nguyami linalounganisha kijiji cha Iyogwe na Gairo, wilayani Gairo.
Ujenzi wa daraja la mfuto (drift) katika mto Nguyami linalounganisha kijiji cha Iyogwe na Gairo, mkoani Morogoro ukiendelea.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Morogoro Mhandisi Godwin Andalwisye (wa pili kushoto), akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias John Kwandikwa (wa pili kulia), kuhusu mradi wa ujenzi wa daraja la mfuto (drift) katika mto Nguyami linalounganisha kijiji cha Iyogwe na Gairo. Mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias John Kwandikwa, akitoa maelekezo kwa mkandarasi M/S Superb Builders And General Supplires (hayupo pichani) anayejenga daraja la mfuto (drift) katika mto Nguyami linalounganisha kijiji cha Iyogwe na Gairo mkoani Morogoro. Daraja hilo linaunganisha barabara ya Iyogwe-Chakwale-Ngilori yenye urefu wa KM 42.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, amemtaka mkandarasi anayejenga daraja la mfuto (drift) katika mto Nguyami linalounganisha kijiji cha Iyogwe na Gairo kuongeza kasi ya ujenzi ili kuwaondolea kero wananchi wa eneo hilo.
Akizungumza na wananchi wa vijiji hivyo mara baada ya kukagua barabara ya Iyogwe-Chakwale-Ngilori yenye urefu wa KM 42, wilayani Gairo, Naibu Waziri Kwandikwa amesema Serikali imejipanga kuhakikisha madaraja matatu muhimu katika barabara hiyo yanakamilika kwa wakati na hivyo kuwezesha shughuli za kiuchumi na uzalishaji.
“Tumejipanga kuhakikisha madaraja yote matatu ya Chakwale, Nguyami na Matale yanakamilika kwa wakati ili kurahisisha shughuli za usafiri na uchukuzi”, amesisitiza Naibu Waziri Kwandikwa.
Awali akitoa taarifa ya mradi wa madaraja hayo, Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Morogoro Mhandisi Godwin Andalwisye, amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa TANROADS imejipanga kukamilisha ujenzi wa madaraja hayo kwa muda uliopangwa.
Madaraja matatu ya Chakwale, Nguyami na Matale yapo kwenye barabara ya Iyogwe-Chakwale-Ngilori yenye urefu wa KM 42 inaunganisha Wilaya za Gairo na Kilindi (Morogoro na Tanga), barabara hiyo ni muhimu kwa kuwa inapita eneo lenye uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula na hivyo kuchochea uchumi wa wakazi wa maeneo hayo.
No comments:
Post a Comment