Ustadh Hajji Khamis akiongoza kisomo cha hitma ya Bi Leyla Mwilima kilicho fanyika Bronx, New York siku ya jumamosi. Bi Leyla alifariki siku ya tar 29 na kuzikwa tar 30 makaburi ya Malborough Muslim Cemetery, NJ. Community ya New York walishiriki kwa pamoja kwenye hitma hiyo na kuwafariji ndugu na familia ya wafiwa kwa kuondokewa na mama yao.
Mwenyekiti wa Community ya New York Bwana Seif Akida alifanikisha hitma hii kama anavyoonekana kwenye picha akisoma dua.
Mume wa Asya na Mkwe wa marehemu Bi Leyla akisoma dua
Dada Sonia akimfariji Asya Mwilima aliekuwa na majonzi kwa kuondokewa na mama mzazi. Kwa taswira zaidi nenda chini.
Dada Asya Mwilima akita shukrani mbele ya wanacommunity walio mbele yake baada ya hitma kusomwa.
Afisa kutoka ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa New York Mzee Hamis akiongea machache kwa niaba ya balozi baada ya hitma.
No comments:
Post a Comment