ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 25, 2019

VIONGOZI WASTAAFU WA MAGEREZA KUZINDUA VITABU VIWILI VINAVYOELEZEA HISTORIA YA JESHI LA MAGEREZA

 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akionesha vitabu viwili ambavyo vimeandikwa na Viongozi Waandamizi wastaafu wa Jeshi la Magereza, akiwemo Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Simon Mwanguku na Naibu Kamishna Mstaafu, John Nyoka, Viongozi hao wamekabidhi vitabu hivyo leo juni 24, 2019, Makao Makuu ya Magereza.  Vitabu hivyo vinaelezea historia ya Jeshi la Magereza pamoja na Programu za Urekebishaji vinatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.
 Viongozi Waandamizi wastaafu wa Jeshi la Magereza,  akiwemo Kamishna Mkuu wa Magereza Mstaafu wa Magereza, Simon Mwanguku(kushoto), Kamishna Mkuu Mstaafu, Jumanne Mangala(katikati) na Naibu Kamishna Mstaafu wa Magereza, John Nyoka(kushoto) wakiwa Ofsini kwa Kamishna Jenerali wa Magereza katika mazungumzo maalum ya maandalizi ya uzinduzi wa vitabu viwili vinavyoelezea historia ya Magereza pamoja na Programu ya Urekebishaji.  
 Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Uwesu Ngarama akiwa na manaibu Kamishna wa Magereza kwa pamoja wakifuatilia mazungumzo maalum ya maandalizi ya uzinduzi wa vitabu viwili vilivyoandikwa na  Viongozi Waandamizi wastaafu wa Magereza, leo Juni 24, 2019.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akizungumza na Viongozi Waandamizi wastaafu wa Jeshi la Magereza(kulia), leo Juni 24, 2019, Makao Makuu ya Magereza. Kushoto ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Uwesu Ngarama akiwa na manaibu Kamishna wa Magereza kwa pamoja wakifuatilia mazungumzo ya maandalizi ya uzinduzi wa vitabu viwili vilivyoandikwa na wastaafu wa Magereza(Picha na Jeshi la Magereza). 

No comments: