Mtu huyo ambaye anahisiwa kuwa mzamiaji na akiwa amebeba chakula na nguo, inaaminika alianguka kutoka katika sehemu ya matairi ya ndege ya Shirika la Ndege la Kenya alikokuwa amejificha, na alianguka muda mfupi kabla ndege hiyo haijatua katika Uwanja wa Ndege wa Heathrow katika jiji hilo.
Safari ya ndege kutoka Kenya hadi London hutumia saa 8 na dakika 50.
Mwaka 2015, mzamiaji aliyejificha sehemu ya chini ya ndege ya shirika la British Airways iliyokuwa ikitoka Johannesburg, Afrika Kusini, alianguka juu ya paa la nyumba moja wakati ndege hiyo ilipokaribia uwanja wa Heathrow, na mtu mwingine aliyekuwa amejificha sehemu hiyohiyo, alilazwa hospitali kutokana na majeraha
No comments:
Post a Comment