ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, July 27, 2019

AZIM DEWJI APATA AJALI AKIELEKEA RUFIJI, ALAZWA MUHIMBILI

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Shia na mfanyabiashara, Azim Dewji, akiwa amelazwa hospitali ya Mchuki Mission, Kibiti.

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Shia na mfanyabiashara, Azim Dewji, na waandishi watatu wa vituo vya televisheni vya ITV, Channel Ten na Azam TV wamepata ajali jana, Julai 27, 2019, asubuhi baada ya gari lao kuacha njia wakati wakiwa njiani kuelekea Rufiji kwenye sherehe za uwekaji jiwe la msingi la mradi mkubwa wa umeme wa MW 2,115 wa Rufiji mkoani Pwani.
Kwa sasa Azim Dewji amelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha mifupa (MOI) akipatiwa matibabu baada ya mfupa wake mmoja wa uti wa mgongo kuvunjika ajalini. Watu wote waliokuwa kwenye gari hilo wametoka salama.
Mwonekano wa gari la Dewji baada ya kupata ajali. GPL

No comments: