Kikundi/ Chama cha
kusaidiana cha Familia Yenye Upendo (Family with Passion-FAWIPA) kilichopo
Nyegezi jijini Mwanza, kimetimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake ambapo hafla ya kusherehekea mafanikio yake imefanyika jana jumapili Juni 30, 2019 ndani ya Passion Hotel.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mwenyekiti wa FAWIPA, Twalib Mafele akizungumza kwenye hafla ya chama hicho iliyofanyika jana ukumbi wa Passion Hotel ikiambatana na harambee kabambe ya kuimarisha chama.
Mgeni rasmi kwenye hafla hioyo alikuwa Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi ambaye aliwakilishwa na Afisa Mtendaji Kata ya Nyegezi, Shaaban Mpuya (katikati).
Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Nyamagana akitoa salamu zake kwenye hafla hiyo.
Mmoja wa wageni waalikwa akitoa nasaha zake kwenye hafla hiyo.
Baadhi ya wageni waalikwa wakitoa salamu zo kwenye hafla hiyo.
Mgeni rasmi akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wanachama wa FAWIPA ambaye alionesha ushiriki mzuri wa shughuli mbalimbali za chama.
FAWIPA ilitoa motisha kwa wanachama wanne walioonyesha ushiriki mzuri wa shughuli mbalimbali za chama.
Washiriki kutoka vyama vingine rafiki pia walialiwa kwenye hafla hiyo.
Wanachama wa FAWIPA pamoja na wageni waalikwa walisimama kwa dakika moja kama ishara ya kumkumbuka
mmoja wa waasisi wa chama hiki, mwanahabari Cathbert Japhet ambaye pia ndiye
aliyependekeza jina la chama kuitwa Familia yenye Upendo, aliyefariki dunia
usiku wa kuamkia Mei 13, 2019.
Wanachama na wageni waalikwa wakiwa ukumbini.
Wanachama na waalikwa mbalimbali wakiwa ukumbini.
Wasaa wa maakuli pia ulikuwepo.
Wasaa wa kusakata rhumba pia ukawadia.
Katibu wa FAWIPA, Innocent Alloyce (kushoto) akiweka kumbukumbu na baadhi ya waalikwa kwenye hafla hiyo.
Tazama Video hapa chini
SOMA>>> Habari mchanganyiko
No comments:
Post a Comment