Mkuu wa msafara huo Mkuu wa Wilaya ya Chato Eng. Mtemi Msafiri akipata maelezo kutoka kwa mkurugenzi wa Rasilimali Misitu na Nyuki TFS, Zawadi Mbwambo jinsi gani wanavyoweza kuzalisha miche ya miti ambayo inakuwa kwa muda mfupi sana
Mkuu wa msafara huo Mkuu wa Wilaya ya Chato Eng. Mtemi Msafiri akiwa na baadhi ya viongozi wa kutoka mkoa wa Geita walipokuwa kwenye ziara ya kutembelea shamba la miti ya kupandwa la Sao Hill lililopo mkoani Iringa
Moja kati ya maeneo ambayo yanatumika kuzalia miche ya miti
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Uchumi wa wilaya ya Mufindi mkoani Iringa umetajwa kutegemea zao
la miti katika kukuza uchumi na kuongeza pato la taifa tofauti ya wilaya
nyingine kama Chato ambao wamekuwa wakitegemea ufugaji,uchimbaji wa dhahabu,uvuvi
na kilimo
Hiyo imebainika wakati wa ziara ya baadhi ya viongozi wa wilaya
ya Chato,Mkoa wa Geita na viongozi wa vijiji vinavyolizunguka Shamba la Miti la
Biharamulo lililopo mkoani Geita baada ya kutembelea Shamba la Miti Sao Hill
linalosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa lengo la
kujifunza shughuli mbalimbali za uendeshaji katika shamba hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa msafara huo Mkuu wa
Wilaya ya Chato Mhe. Eng. Mtemi Msafiri alisema kuwa kwa mara ya kwanza
amejifunza faida kubwa inayotokana na zao la miti katika kukuza uchumi wa nchi
na kujionea jinsi gani wananchi wa wilaya ya Mufindi wanavyonufaika na dhahabu
ya kijani
“Leo ndio nimegundua kuwa zao la miti ni dhahabu ya kijani kwa
namna inavyosaidia kukuza uchumi tofauti na walivyodhani hapo awali kwa namna
ambavyo wao wamekuwa wakitegemea kuchimba dhahabu ambazo hazionekani tofauti na
zao la miti ambavyo limekuwa linaonekana” alisema Eng Msafiri
Eng Msafiri alisema kuwa shamba la Miti Sao Hill ndilo shamba
kubwa zaidi kati ya mashamba yote ya Serikali na ni nguzo ya maendeleo, na
mkombozi wa mazingira wa Wilaya ya Mufindi na mikoa ya Nyanda za Juu Kusini
nasi tumeona ni vema tujifunze kutoka kwa wenzetu.
“Tumejionea jinsi shamba hili lilivyo kuwa dhahabu ya ukuaji wa
sekta ya viwanda vidogo na vikubwa vya uchakataji wa mbao, linavyosaidia
kuongezeka kwa ari ya upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira kwa wananchi
wanaozunguka shamba na wananchi wa Wilaya za Mufindi, Kilombero na jamii jirani
wamekuwa wakipatiwa gawio la asilimia 5 ya mrahaba kila mwaka”alisema Eng.
Msafiri.
Eng. Msafiri anasema ziara hiyo imeweza kuwafumbua macho na
kuona jinsi gani shamba hilo lilivyo toa fursa ya ajira zinazotokana na
kazi za msimu za mashambani na viwanda tegemezi vya mazao ya misitu, fursa za
uwekezaji, na ufugaji wa nyuki unaotokana na na uwepo wa misitu ya asili
na ile ya kupandwa pamoja na vyanzo mbalimbali vya maji.
Awali akitoa ufafanuzi wa shamba la Sao Hill mkurugenzi wa
Rasilimali Misitu na Nyuki TFS, Zawadi Mbwambo alisema shamba hilo ni
miongoni mwa mashamba 23 ya miti ya kupandwa ya serikali ambayo yanasimamiwa na
wizara ya maliasili na utalii kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).
“Shamba la Sao Hill lililopo hapa Mufindi lilianzishwa kwa
majaribio mnamo mwaka 1939 hadi mwaka 1951 na upandaji kwa kiasi kikubwa
ulianza rasmi mwaka 1960 hadi 1980 na
shamba hilo linaukubwa wa hekta 135,903 ambazo zimehifadhiwa kwa ajili ya
upandaji wa miti na uhifadhi wa
mazingira” alisema Mbwambo
Mbwambo alisema shamba hilo limehamasisha kwa kiwango kikubwa
upandaji wa miti kwa jamii inayolizunguka ambapo pia hutoa msaada wa mafunzo na
miche ya miti kwa ajili ya kupandwa ili kupambana na uharibifu mkubwa wa misitu
unaoendelea nchini.
“Takribani hekta 372,000 ya misitu inapotea kila mwaka na
ili misitu hii isiweze kupotea tunatakiwa tuendelee kupanda angalau hekta
185,000 kwa mwaka kwa hapa Mufundi na Ukanda wote wa Nyanda za Juuu Kusini
hamasa ya kupanda miti imekuwa kubwa kutokana na thamani inayoonekana Sao Hill
kiasi kwamba imefikia hatua sasa Serikali inawaelimisha watu waache baadhi ya
maeneo kwa ajili ya kilimo cha mazao mengine ya chakula na biashara” Alisema
Mbwambo.
Kwa upande wake meneja wa Shamba la Miti la Biharamulo Thadeus
Shirima alisema kupitia ziara hiyo ya siku mbili anaamini sasa kutakuwa na
uelewa wa pamoja wa umuhimu wa shamba hilo katika kuleta maendeleo katika Kanda
ya Ziwa na Tanzania kwa ujumla.
Thadeus alitoa shukurani kwa Mkuu wa Wilaya ya Chato, kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Wilaya Chato na Mkoa wa Geita, Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Chato na Bukombe kwa msaada na maelekezo yao muhimu
yaliyosaidia kuhakikisha uanzishwaji wa Shamba la Miti la Biharamulo
unafanikiwa kwa kufanikisha kuwaondoa wananchi waliovamia msitu wa hifadhi
Biharamulo ili kuanzishwa shamba hilo la miti.
Ziara hiyo ina wajumbe 45 ambao vingozi wa Wilaya na Mkoa wa
Geita, Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Mkurugenzi wa halmashauri,Wenyeviti wa
Vijiji, Madiwani, Maafisa tarafa, Jeshi la Zima moto na uokoaji, Mwenyekiti na
katibu wa Chama cha Mapinduzi, baadhi ya Wakuu wa Vitengo na Idara za
Halmashauri ya Wilaya, baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya
Wilaya , Katibu Tawala wa Wilaya na Wataalamu kutoka Shamba la miti
Biharamulo.
No comments:
Post a Comment