ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, July 2, 2019

Watanzania walio nje ya nchi hawataandikishwa

By Noor Shija, Mwananchi

“Sheria za Nec haziruhusu uandikishaji wapigakura nje ya nchi.” Ndilo jibu la Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Jaji Semistocles Kaijage alipojibu swali kuhusu Watanzania walio nje ya nchi.

Swali hilo lilitokana na mada kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk Athumani Kihamia kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari.

Muuliza swali alitaka kufahamu sababu za kutokuwapo kipengere cha namna gani Watanzania watakaokuwa nje kikazi au kwa dharura zingine ikiwamo kupata matibabu wataweza kuandikishwa.

Jaji Kaijage akijibu swali hilo alisema sheria inawataka kuboresha daftari la wapigakura mara mbili, baada ya uchaguzi mkuu unaomalizika na kabla ya uchaguzi mkuu mwingine.

Hivyo, anasema kwa wale watakao kuwa nje ya nchi wakati wa uboreshaji wa daftari, wanaweza kujiandikisha wakati mwingine. Hata hivyo, muuliza swali aliomba ufafanuzi zaidi kwa maana swali lake haliwahusu Watanzania wanaoishi nje, bali kwa wale waliokwenda kwa safari za muda mfupi, kikazi au dharura.

Muuliza swali alifafanua kwamba kwa sasa Nec inajiandaa kuandikisha wapigakura wapya na wale wanaotaka kuboresha taarifa zao kama vile kuhama makazi au kubadili jina au kuna wengine kadi zao zimepotea na sasa wanataka mpya, itakuwaje kwa Mtanzania aliyekwenda safari ya muda mfupi nje ya nchi.

No comments: