ANGALIA LIVE NEWS

Friday, August 2, 2019

JK AUNGANA NA WANA MSOGA KUUPOKEA MWENGE WA UHURU

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amebeba Mwenge wa Uhuru wakati ulipowasili kijijini Msoga, Agosti 1, 2019.
Dkt. Kikwete aliwaongoza wanakijiji wa Msoga kushiriki mbio za mwenge wakati ulipopita kijijini hapo akiwemo pia Mkewe Mama Salma Kikwete, Mbunge wa Chalinze Mhe. Riziwani Kikwete, Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainab Kawawa. na viongozi wengine wa wilaya ya Bagamoyo.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Zainab Kawawa akizunguzma wakati wa hafla hiyo.
Dkt. Kikwete, mkewe Mama Salma Kikwete na Kiongozi wa Mbio za Mwenge, Mzee Mkongea Ally
Rais Mstaafu Dkt. Kikwete, (watatu kushoto), mkewe Mama Salma, (wapili kushoto) Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu (wane kushoto) na viongozi wengine wa Kijiji cha Msoga, wakisubiri mwenge wa Uhuru uwasili kijijini hap Agosti 1, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwengewa Uhuru, Mzee Mkongea Ally, akizungumza baada ya mBio za Mwenge kuwasili kijijini Msoga

No comments: