Afisa Tarafa Itiso Remidius Emmanuel akionyesha Stakabadhi ya Shilingi Milioni Moja iliyorejeshwa katika akaunti ya maji baada ya kamati ya maji kushikilia fedha hiyo kinyume na taratibu.
Juma Mohamedi Moja ya wananchi wa Kitongoji cha Wali akiwasilisha kero yake kwa Afisa Tarafa -Itiso Remidius Emmanuel katika mkutano huo.
Mwananchi wa Kitongoji cha Wali Emmanuel Panga akisoma taarifa ya Mapato na Matumizi kwa niaba ya kamati ya Maji.Taarifa ambayo hata hivyo haikupokelewa na Afisa Tarafa.
Baadhi ya wananchi wa Kitongoji cha Wali walioshiriki Mkutano huo.
Afisa Tarafa Itiso Remidius Emmanuel akiwa na viongozi wa ngazi ya Kata, Kijiji na Kitongoji husika
AFISA Tarafa wa Itiso, wa wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Remidius Emmanuel amewahamasisha wananchi wa tarafa hiyo kuendelea kujiandikisha katika orodha ya Daftari la Wapiga kura kwa kutambua thamani yaa kuchagua viongozi wa Kijiji na Kitongoji chao katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novenba 24 mwaka .
Afisa Tarafa huyo ameyasema hayo wakati akiwa katika ziarani katika Kitongoji cha Wali (Kijiji cha Izava) kwa lengo la kuhamasisha wananchi hao kuendelea kujiandikisha katika orodha ya Daftari la Wapiga kura, ameesema kuwa serikali inapanga maendeleo yake kuanzi ngazi ya mtaa, Kijtongoji pamoja na Kijiji.
"Nyinyi ni mashahidi, wengi tumeshuhudia na kusikia Oktoba 12 mwaka huu katika ardhi hii ya Wilaya ya Chamwino Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Pombe Joseph Magufuli alijiandikisha katika Kituo cha Sokoine (Chamwino Ikulu), Mheshimiwa Mkuu Wa wilaya yetu nae ameisha jiandikisha,mimi Afisa Tarafa wenu tayari nimejiandikisha, Sasa ni zamu yenu kujiandikisha kwa wingi wale ambao hawajashiriki zoezi hili.amesema Afisa Tarafa huyo.
Katika hatua nyingine Afisa Tarafa huyo ameikataa taarifa ya Mapato na Matumizi ya Kijiji cha Izava iliyosomwa mbele yake baada ya wananchi kulalamika kwa kipindi kirefu pasipo kusomewa mapato na Matumizi ya mradi wa Maji Kitongojini hapo baada ya Afisa huyo kuwataka wananchi waseme kero zote zinazowakabili.
Emmanuel amesema kuwa viongozi tunapaswa kuwajibika na kutendea haki nafasi na nyadhifa tulizo nazo, mambo haya ya kushindwa kusoma taarifa za mapato na matumizi ni tafsiri ya baadhi yetu kushindwa kutimiza wajibu wetu na kuwafanya wananchi kupunguza imani na viongozi wao.
Amesema wananchi wachague viongozi ambao watakuwa wanasoma mapato na matumizi kwa wakati na kuweza kufanyika maendeleo kutokana na miradi inayoendelea.
Hata hivyo Afisa tarafa huyo alikataa kuipokea taarifa iliyosomwa mbele yake na kamati hiyo na kuagiza iandaliwe taarifa nyingine itakayotoa mchanganuo sahihi pamoja na nyaraka muhimu ili wananchi hao waweze kusomewa taarifa sahihi ya mradi huo.
" Mfano,nimesikia kuna mahala hapa taarifa inaonyesha kwamba wajumbe walienda kufungua akauti ya Maji Dodoma na walitumia Tsh.400,000/=, Yaani kwenda Dodoma na kufungua akauti mnatumia kiasi hiki cha fedha ?..Sasa nataka iandaliwe taarifa nyingine na iwe na mchanganuo wa mapato na matumizi ya fedha hizi ili wananchi wafahamu na lazima muweke na nyaraka zitakazoonyesha uhalisia wa matumizi hayo" Amesema Afisa Tarafa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya Maji Amosi Mainaa Lugumbau aliwaomba radhi wananchi hao baada ya kukiuka makubaliano ya awali na kushindwa kuwasilisha taarifa za mapato na matumizi kwa wananchi wa kitongoji hicho pamoja na kutohusisha uongozi wa kijiji katika shughuli zote za mradi huo.
Katika ziara yake, Afisa Tarafa aliambatana na Mtendaji wa kata ya Segala Bi.Twahia komba pamoja na viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Izava.
No comments:
Post a Comment