Wapili toka kushoto ni Asha Nyang.anyi akiwa na ndugu, jamaa na marafiki waliojumuika katika hitma ya arobaini ya mpendwa kaka yao Hussein iliyofanyika siku ya Jumamosi Oct 19, 2019 Sandy Spring. Maryland nchini Marekani na kuhudhuriwa na wanaDMV wakiwemo marafiki zao kutoka majimbo mengine. PICHA ZOTE NA ISKA JOJO STUDIO. www.iskajojostudios.com
Kushoto ni Dkt. Rahma Nyang'anyi akiwa pamoja na Joha Nyang;anyi (watatu toka kushoto) wakijumuika pamoja na ndugu, jamaa na marafiki kwenye kisomo cha hitma ya arobaini ya kaka yao Hussein iliyofanyika siku ya Jumamosi Oct 19, 2019 Sandy Spring. Maryland nchini Marekani
Kisomo cha hitma ya arobaini ya mpendwa kaka Hussein Nyang'anyi ikiendelea.
Kulia ni mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada Meja Jenerali Adolph Mutta pamoja nae ni Prof Nicholas Boas wakifuatilia kisomo.
Swala ya magharib ikifanyika kabla ya kisomo kuanza.
Swala ya magharib ikiendelea.
Sheik akitoa mawaidha baada ya kisomo.
Saleh mmoja ya wanafamilia akiongea machahe.
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada Meja Jenerali Adolph Mutta akitoa salamu kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Aliyekua balozi wa Tanzania nchini Marekani, Balozi Liberata Mulamula akiongea machache jinsi alivyomfahamu Hussein na jinsi gani Hussein alivyokua akimpigia simu hata usiku wa manane. Kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Mojomba wa familia mkuu wa Wilaya Springfield, Massachusetts Ankal Kibodya akiongea kwa niaba ya familia.
Dkt. Hamza Mwamoyo akiongea na kumuelezea Hussein alikua ni mtu wa aina gani katika jumuiya.
Rais wa Jumuiya Dj Luka kwa niaba ya uongozi wa Jumuiya ya waTanzania DMV akitoa pole kwa makamu wa Rais wa ATC Joha Nyang'anyi na familia yake na kuwashukuru wanaDMV kwa kujitokeza kwa wingi na kujumuika na wafiwa kwani hiyo ni faraja kubwa kwa familia.
Mwenyekiti wa TAMCO Ally Mohammed kwa niaba ya TAMCO akitoa shukurani nyingi na kutoa maelekezo ya kutoa sadaka ambayo ilipatikana zaidi ya $500 ambayo itapelekwa kwenye vituo vinavyolea yatima nchini Tanzania.
Picha juu na chini wanaDMVna marafiki zao kutoka majimbo mengine wakitoa pole na kupiga picha ya pamoja na wafiwa.
WaTanzania kutoka majimbo mengine wakiwa katika picha ya pamoja na wafiwa
No comments:
Post a Comment