Tangazo rasmi la Serikali lilisema kuwa Sineenat alikuwa mwenye tamaa na alijaribu kujiweka katika hadhi ya malkia.
“Tabia ya ya mke wa mfalme zilichukuliwa kama ukosefu wa heshima,” ilisisitiza taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa Shirika la habari la Reuters, Sineenat ambaye alikuwa meja jenerali na rubani wa ndege za kivita, muuguzi na mlinzi alikuwa mtu wa kwanza kutunukiwa cheo cha mke Mtukufu wa Ufalme
Malkia Suthida mwenye umri wa miaka 41 ambaye alikuwa mhudumu wa zamani wa ndege na naibu mkuu wa kikosi cha walinzi wa kifalme alikuwa mpenzi wa muda mrefu wa Mfalme Vajiralongkorn.
Inaelezwa kuwa miaka mingi mara kwa mara amekuwa akionekana kando ya Mfalme Vajiralongkorn na aliaminiwa kuwa ndiye mtu aliyekuwa karibu nae kuliko mtu mwingine lakini sasa amevuliwa rasmi cheo hicho.
Habari zaidi zinasema kuwa hata baada ya kumuoa malkia Suthida, bado Sineenart alikuwa ndiye mtu aliyeonekana zaidi na kuheshimika katika matukio ya kifalme.
Tangazo la kuvuliwa vyeo kwa Sineenat lilichapishwa katika jarida la Ufalme Jumatatu iliyopita na kueleza kuwa kuanguka kwake kutoka cheo cha juu katika ufalme wa Thailand ni mabadilikoya ghafla ya hadhi yake ya juu aliyokuwa nayo ndani ya Ufalme.
Sababu za kung’olewa
Tangazo hilo lilisema “alionyesha pingamizi na shinikizo kwa njia zote katika kuzuia uteuzi wa Malkia kabla ya harusi ya mwezi Mei.
“Mfalme alimpatia cheo cha mshauri wa ufalme akiwa na matumaini ya kuondoa msukumo na matatizo ambayo yangeweza kuathiri ufalme,” lilisema tangazo hilo. GPL
No comments:
Post a Comment