ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, October 23, 2019

NAIBU WAZIRI MABULA AAGIZA KUFICHULIWA MASHAMBA PORI ILI YAFUTWE

 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halamashauri ya Wilaya ya Moshi Kastori Msigala baada ya kukagua Majalada ya Ardhi katika Ofisi za Ardhi za Halamashauri hiyo jana wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta hiyo mkoani Kilimanjaro. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kippi Warioba.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Kastori Msigala kabla ya kuondoka jana wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta hiyo mkoani Kilimanjaro. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kippi Warioba.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi na Nyumba za Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) katika shamba la Miti la Kilimanjaro Kaskazini (Rongai) uliopo wilayani Rombo mkoa wa Kilimanjaro jana wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo. Kulia ni Mhandisi wa ujenzi wa mradi huo kutoka Shirika la Nyumba la Taifa Peter Mwaisabula.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akioongozwa na Kaimu Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Kilimanjaro Stanley Msoffe (Kulia) kwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi na Nyumba za Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) katika shamba la miti la Kilimanjaro Kaskazini (Rongai) uliopo wilayani Rombo mkoa wa Kilimanjaro jana wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na wafanyakazi wanaojenga nyumba za watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika shamba la miti la Kilimanjaro Kaskazini (Rongai) lililopo Rombo mkoa wa Kilimanjaro wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi na Nyumba za TFS jana wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo.

Na Munir Shemweta, WANMM KILIMANJARO
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameziwataka idara za ardhi katika halmashauri nchini kuyabainia mashamba yote yasiyoendelezwa (Mashamba Pori) na kupeleka mapendekezo ya kufutwa mashamba hayo Wizarani.

Dkt Mabula alisema hayo jana alipokutana na watendaji wa sekta ya ardhi pamoja na wakurugenzi wa halamashauri zote za mkoa wa Kilimanajaro akiwa katika zaiara yake ya siku mbili mkoani humo kukagaua utendaji kazi wa sekta ya adhi.

Dkt Mabula alisema, pamoja na baadhi ya mashamba kufutwa katika maeneo mbalimbali nchini kutokana na kutoendelezwa lakini kuna maeneo mengine maafisa ardhi wameshindwa kuyatolea taarifa mashamba yasiyoendelezwa ili yafutwe kwa sababu wanazozijua wenyewe.

‘’Nataka taarifa ya mashamba yote pori katika halmashauri yabainishwe na kutolewa taarifa ili tuweze kupeleka mapendekezo ya kufutwa mashamba hayo kwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’’ alisema Dkt Mabula

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, taarifa ya kubaini mashamba yote pori katika kila halmashauri ziwe zimewasilishwa kufikia desemba mwaka huu na Januari 2010 timu maalum itaundwa kwa ajili ya kazi hiyo.

Dkt Mabula alisema, Afisa Ardhi katika halmashauri yoyote atakayebainika kuficha ukweli kuhusiana na uwepo mashamba pori katika eneo lake hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.

‘’Maafisa Ardhi mnashirikiana na baadhi ya wenye mashamba pori na mnashindwa kuleta mapendekezo ya kufutwa mashamba, sisi tunahitaji kuona kila ardhi inatumika katika malengo yaliyokusudiwa’’ alisema Dkt Mabula

Mapema katika kikao hicho, baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri za mkoa wa Kilimanajaro pamoja na Maafisa Ardhi alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa, idara za ardhi katika halmashauri zao zinakabiliwa na changamoto kubwa za upungufu wa watumishi katika fani tofauti za sekta ya ardhi pamoja na bajeti finyu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi Kastori Msigala alieleza kuwa halmashauri yake inakabiliwa na upungufu wa watumishi katika fani za Mipango Miji, Upimaji na Uthamini jambo alilolieleza kuwa linachangia kwa kiasi kikubwa kutofikia malengo katika sekta ya ardhi.

Katika hatua Nyingine Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Ofisi na Nyumba za Wakala wa Huduma za Misitu TFS katika Shamba la Miti la Kilimanjaro Kaskazini maarufu kama Rongai lililopo wilayani Rombo mkoa wa Kilimanjaro

Kwa mujibu wa Kaimu Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Kilimanjaro Stanley Msoffe, Ujenzi wa Ofisi na Nyumba za Watumishi wa TFS unaofanywa na NHC unagharimu zaidi ya milioni 532.9 unatarajiwa kukamilika mwezi Juni 2020.

No comments: