Sunday, October 20, 2019

WAZIRI MKUU MAJALIWA AONDOKA NCHINI KUELEKEA RUSSIA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Oktoba 20, 2019 ameondoka chini kwenda Urusi ambako atamwakilisha Rais Dkt.John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika na Russia. Pichani, Waziri Mkuu akisalimiana na Spika wa Bunge Job Ndugai kwenye Uwanja Ndege wa Julius Nyerere kabla ya kuondoka. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Oktoba 20,2019 amekutana na Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Wizara ya Kilimo katika kikao cha kazi kilichofanyika kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam. Pichani, Waziri Mkuu akizungumza na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (wa pili kulia), Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba (wa tatu kulia), Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe (wa pili kushoto), Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe, na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Profesa Siza Tumbo. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments: