SERIKALI imesema itaandelea kufanya oparesheni ya uhujumu uchumi ili kudhibiti utengenezaji na upatikanaji wa fedha bandia katika maeneno mengi nchini na itahakikisha kuwa inatoa elimu juu ya madhara ya uingizwaji wa fedha bandia katika mzunguko fedha hizo.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florence Luoga amsema kuwa mwananchi yeyote afanyae kazi ya kutengeneza au kumiliki fedha bandia ni kosa la jinai na akibainika sheria itachukua mkondo wake.
“Kupatikana na noti bandia ni kosa ambalo halihitaji ushahidi, maana wewe unayepatikana na noti au fedha haramu baada ya hapo unapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria na ufungwe, kwa hiyo wakati wa elimu ya noti bandia inatolewa nawatahadharisha wananchi wanatakiwa kuhakikisha hawapatikani na noti au fedha haramu”, Alisema Prof. Luoga.
Alisema kuwa wahujumu uchumi wanaweza wakaharibu uchumi kwa kuchagiza mfumuko wa bei kuwa kuingiza fedha haramu katika mzunguko wa fedha za nchi hali ambayo inamadhara makubwa sana kiuchumi.
Aidha aliwapongeza vyombo vya dola kwa kushirikiana katika mapambano ya kuondoa fedha bandia katika mzunguko wa uchumi kwa kukamata waharifu wanajihusisha na utengenezaji wa fedha bandia kule Chanika Jijini Dar es Salaam, aliongeza kuwa Benki Kuu ina fedha za kutosha za kigeni ambazo zinaweza endesha uchumi bila shida yoyote.
“Sasa hivi nchi yetu ina fedha za kutosha za kigeni hata yale mazoea ya kutishiwa kuwa nchi haina fedha za kigeni za kutosha kwa hiyo hatuwezi kuendesha shughuli zetu hilo siyo tatizo kwa sasa kwea nchi yetu kwani kwa sasa tunapesa za kutosha”, Alisisitiza Prof. Luoga.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alisema kuwa mnamo Desemba 15, mwaka huu Jeshi la Polisi lilimkamata mkazi wa Chanika Jijini Dar es Salaam na wenzake wawili wakijihusisha na uendeshaji wa kiwanda cha kutengeneza noti bandia.
“Jeshi la Polisi na Wadau wengine wa Masuala ya ulinzi na usalama pamoja na Menejimenti ya BOT tumeweza kuiwakamata waharifu sugu wanaojihusha na uendeshaji wa kiwanda cha kutenegeneza noti bandia na tukakamata noti bandia za nchi mbalimbali ambazo wametengeneza”, Alisema Kamanda Mambosasa.
Mambosasa alisema kuwa oparesheni hii ilianzia Wilayani Hai baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo Lengai Ole Sebaya kukamata noti bandia Zaidi ya shilingi milioni 11, huku kwa Dar es Salaam zikikamatawa noti za kitanzania 10,540, dola za marekani 133, 048, Msumbiji noti 110,23, Congo DRC noti 2,270, Kenya noti 1 pamoja na Malawi noti 1.
No comments:
Post a Comment