IGP Sirro amesema hayo leo jijini Dar es salaam, wakati alipofanya ziara ya ukaguzi na kutembelea vikosi vinne vilivyopo chini ya Jeshi hilo ikiwemo Kikosi cha Polisi Tazara, Reli, Ufundi pamoja na Kikosi cha Polisi Wanamaji.
Aidha, IGP Sirro amesema kuwa, ziara yake imelenga katika kufanya tathimini ya kiutendaji kutokana na kazi kubwa inayofanywa na Makamanda pamoja na wasaidizi wao.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli la Tazara Bruno Ching’andu ameeleza kuwa, wameendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi na kwamba ushirikiano huo umesaidia kupunguza matukio ya uhalifu ikiwemo kuhujumu njia ya treni pamona na vitendo vingine vya rushwa.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania TRC Masanja Kadogosa amesema kuwa, mbali ya kuwepo kwa changamoto kadhaa ikiwemo za baadhi ya watu kujihusisha na uhalifu lakini wameweza kudhibiti vitendo hivyo kutokana na ushirikiano uliopo kati yao na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (kushoto) akiweka saini kitabu cha wageni wakati alipofanya ziara ya ukaguzi katika Kikosi cha Polisi Tazara na kukutana na Menejimenti ya Shirika la Reli la Tazara leo Jijini Dar es salaam, wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli la Tazara Bruno Ching’andu. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa, wakati alipofanya ziara ya ukaguzi katika Kikosi cha Polisi Reli na kukutana na Menejimenti ya Shirika la Reli la Tanzania TRC leo Jijini Dar es salaam. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akizungumza na baadhi ya askari wa Kikosi cha Polisi TAZARA wakati alipofanya ziara ya ukaguzi kwenye kikosi hicho kwa lengo la kufanya tathmini ya kiutendaji kutokana na kazi kubwa inayofanywa na Makamanda pamoja na wasaidizi wao. Picha na Jeshi la Polisi.
Askari wakitoa salamu ya kijeshi mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, kwenye gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake wakati alipofanya ziara ya ukaguzi katika kikosi Polisi Tazara na Kikosi cha Reli kwa lengo la kufanya tathmini ya kiutendaji kutokana na kazi kubwa inayofanywa na Makamanda pamoja na wasaidizi wao. (Picha na Jeshi la Polisi).
No comments:
Post a Comment