ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, December 21, 2019

KONGAMANO LA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI LAENDELEA ARUSHA

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw. Richard Kwitega akikagua bidhaa za wanawake wajasiliamali jana Mkoani Arusha wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi linaloendelea Jijini Arusha kushoto kwake ni Mboni Mgaza Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya familia kutoka Wizara ya Afya.
Mwanamke Mjasiliamali akifafanua jambo kuhusu bidhaa ya wine inayotengenezwa kiwandani kwake kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw. Richard Kwitega wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi linaloendelea Jijini Arusha kushoto kwake ni Mboni Mgaza Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya familia kutoka Wizara ya Afya.
Baadhi ya wanawake walioshiriki katika Kongamano la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi wakifutilia jambo wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo jana Arusha.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw. Richard Kwitega akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanawake wajasiliamali jana Mkoani Arusha mara baada ya ufunguzi wa Kongamano la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi linaloendelea Jijini Arusha.
………………………
Na Mwandishi Wetu Arusha
Serikali inatambua kuwa haiwezi kufikia malengo ya maeandeleo endelevu ikiwa wanawake hawatashiriki na kunufaika na uchumi kama ilivyo kwa wanaume kwasababu mfumo dume hautoshi kuiletea Nchi maendeleo.
Hayo yamesemwa leo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw. Richard Kwitega wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi linaloendelea Jijini Arusha.
Bw. Kwitega ameongeza kuwa ili kuwa na maendeleo endelevu ni lazima kuwashirikisha wanawake kiuchumi ili kunuafaika na uchumi au matokeo ya shughuli za Maendeleo.
Aidha Bw. Kwitega aliongeza kuwa kwa kuzingatia dhamana ya Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii ya uratibu na wa masuala ya usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake kiuchumi inaendelea na maandalizi ya sera ya Jinsia ili kuhakikisha mipango yote inazaingatia usawa wa kijinsia.
Bw. Kwitega ameitaja mikakati na mipango ya maendeleo ya Taifa pamoja na mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto kuwa mipango yote iliyopo inaielekeza Serikali kuwezesha wanawake kiuchumi.
Kiongozi huyo wa Mkoa wa Arusha amezija juhudi za serikali katika kuhakikisha wanawake wanakua kiuchumi kuwa ni kuhamasisha wanawake kujiunga VICOBA na SACCOS na vikundi vingine vya hisa na kuongeza kuwa mpaka sasa serikali ina vikundi 918 venye jumla ya Wanawake 10,708 wamejiunga na vikundi hivyo Nchi nzima.
Naye Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Mboni Mgaza amesema lengo kuu la Kongomano la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi ni kuwatayarisha wanawake Mkoani Arusha pamoja na Taasisis zinazojishughulisha na uwezeshaji wanawake kuweza kuwajenga uwezo wa kiuchumi.
Bi. Mgaza amezitaja mbinu zinazotumika kujengea uwezo wa wanawake kiuchumi ni pamoja na kuwapa mitaji na mikopo lakini pia kuwapa ujuzi wa teknolojia na kujenga ubia baina ya Serikali na Taasisi mbalimbali.
Bi. Mboni aliongeza kuwa Kongamano hilo la wanawake linalenga vikundi vya kiuchumi, vikundi vya ujasiliamali pamoja na watu binafsi zikiwemo taasisi mbalimbali Mkoani Arusha kwa lengo la kupata maarifa mbalimbali ya kujikwamua kiuchumi.


Serikali imekuwa ikitoa Mikopo kupitia Serikali za Mitaa kwa Wanawake waliokatika vikundi vya hisa na ujasiliamali kwa lengo kuwezesha wanawake kiuchumi na tayari Serikali tayari kupitia mapato ya Halmashauri zote Ncini inatenga asilimia kumi ya mapato yake kwa lengo la kuwezesha wanawake vijana na walemavu.

No comments: