Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Fortunatus Muslim akizungumza na madereva katika stendi kuu ya mabus ubungo Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Madereva na wa mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani wakiwa wamekusanyika waimsikiliza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Fortunatus Muslimu
Madereva na mawakala wa mabasi ya abiria wakimsikiliza Kamanda wa Kikosi cha usalama Barabarani nchini Fortunatus Muslim
Kamanda wa Kikosi cha usalama Barabarani Nchini Fortunatus Muslim akijibu maswali yaliyoulizwa na baadhi ya wadau wa usafirishaji abiria katika stendi ya mabus ubungo.
Akisisitiza madereva wa mabasi ya abiria kuacha mara moja kuwashusha abiria porini ili wakajisaidie (almaarufu kuchimba dawa)badala yake wawapeleke abiria sehemu ambayo watapata huduma nzuri ya choo.
Kamanda wa Kokosi cha Usalama Barabarani Fortunatus Muslim akisisitiza jambo.
Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Fortunatus Muslim akijibu maswali ya wadau wa Usafirishaji abiria katika stendi kuu ya mavasi ubungo.
Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Nchini Fortunatus Muslimu akitoa ufafanuzi wa jambo kwa wadau wa Asasu za kiraia zinazojihusisha na shughuli za usalama barabarani
Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini Kamanda Fortunatus Muslim akiendelea kutoa ufafanuzi wa maswali aliyoulizwa.
Kamanda Kikosi cha Usalama barabarani nchini Fortunatus Muslim akiwa katika picha ya Pamoja na mabalozi wa usalama barabarani RSA katika stendi ya mabus Ubungo.
Na Vero Ignatus, Dar
Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kwa kushirikiana na Asasi za kiraia zinazoshughulika na usalama barabarani ikiwemo RSA wametoa elimu kwa madereva katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani ubungo jijini Dar es salaam
Akizungumza katika kampeni hiyo inayofahamika kama abiria paza sauti
Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Forturnatus Muslim amewataka madereva kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani wawapo safarini
Kamanda Muslim amewataka madereva hao kuwa timamu punde wanapotaka kulipita gari lingine barabarani lazima wawe na uhakika kuwa mbele hakuna gari jingine lililoruhusiwa kulipita gari jingine ili kuepusha ajali waambazo zinaweza kuepukika.
''Nimeshuhudia naona madereva wa baadhi ya makampuni ya mabaasi anaovateki mabasi matatu na malori mawili ,hivi kweli barabara zetu hizi utaovatake mabasi matatu na malori mawili,hujakutana na gari lingine kule mbele?''aliuliza.
Sambamba na hilo amewataka madereva wa mabasi ya abiria kuacha mara moja kuwashusha abiria porini ili wakajisaidie (almaarufu kuchimba dawa)badala yake wawapeleke abiria sehemu ambayo watapata huduma nzuri.
''Hakikisha unawashusha abiria wako wanapata huduma katika maeneo maalum ya ambayo yanahuduma ya choo siyo porini huko,mnayoita kuchimba dawa watu wachimbe sehemu sahihi na salama ili kuepusha mlipuko wa magonjwa ''Alisisitiza
Akizungumza Mratibu wa Kanda ya Mashariki (RSA) Augustino Jonas Mkumbo amewataka madereva kufahamu kuwa udereva ni taaluma ndiyo maana wanaingia darasani kuisomea.
Hivyo amewataka madereva kutambua kuwa ni jukumu lao kkufuata taaluma hiyo kwa vitendo kwa kufuata na kuzungatia sheria na kanuni za usalama barabarani ili abiria waweze kuwa salama wakati wote pamoja na vyombo vya moto kutokusababisha ajali zinazoweza kuepukika.
Kwa upande wake Katibu wa chama cha waathirika kwa ajali za barabarani (DPDO)Kombo Jumbe kutoka Dodoma amesema kuwa ananchi hawawezi kufanya kazi kama madereva watawasababisha ajali ambazo zinawapelekea vifo au ulemavu wa kudumu.
Amewaomba madereva kuchukua hatua pale wanapoona chombo hakipo salama wawaambie wamiliki ili kiweze kufanyiwa matengenezo kabla ya kusababisha ajali.
''Hata mimi nilikuwa nafunga kiatu kama ninyi ila ajali ndiyo imesababisha haya yote mnayoyaona nilipoteza miguu yangu yote miwili mika minne iliyopita''alisema Kombo
Amewataka madereva kujitahidi kuepusha ajali ili watu waweze kusafiri salama na kufika kule wanakoelekea salama,ili waweze kufanya kazi na kukuza uchumi kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment