ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 20, 2019

RAIS MAGUFULI AFUNGUA MRADI WA VISIMA VIREFU PAMOJA NA UJENZI WA MADARASA SHULE YA MSINGI CHATO A-B MKOANI GEITA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi mbalimbali akifungua moja ya mradi wa Kisima kirefu kilichojengwa katika Shule ya Msingi Chato A-B kwa ufadhili wa Emirates Red Crescent-UAE kwa usimamizi na Utekelezaji wa Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania katika sherehe zilizofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Chato A-B Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi waChato katika sherehe za Ufunguzi wa Madarasa yaliyojengwa kwa mchango wake Mhe. Rais Dkt. Magufuli pamoja na mradi wa Visima virefu vya Maji vilivyojengwa na Emirates Red Crescent-UAE kwa usimamizi na Utekelezaji wa Balozi wa Falme za Kiarabu nchini
Tanzania zilizofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Chato A-B Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa Shule ya Msingi Chato A-B mara baada ya kufungua Madarasa pamoja na Ofisi zilizojengwa kwa Mchango wake mwenyewe katika shule hiyo ambayo alisoma elimu yake ya Msingi. Sehemu ya Madarasa ya Shule ya Msingi Chato A-B kama yanavyoonekana mara baada ya ujenzi wake kukamilika. PICHA NA IKULU

No comments: