ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 20, 2019

UWEZESHAJIWANAWAKE KIUCHUMI NI NYENZO MUHIMU YA KUONDOKANA NA UKATILI WA KIJINSIA

Mshauri Mwelekezi wa mapitio ya Sera ya Taifa ya Jinsia Profesa Linda Mhando akikifanua jambo kwa Washiriki wa Kikao Kazi cha kutoa maoni na tathimini ya Sera ya Taifa ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 2000.
Baadhi ya Washiriki wa Kikao Kazi cha kutoa maoni na tathimini ya Sera ya Taifa ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 2000 wakifuatilia jambo mapema laeo Jijini Arusha.

Na Mwandishi wetu Arusha.
Kuwawezesha wanawake kiuchumi ni njia mojawapo inayofanya wanawake wengi nchini kuepukana na unyanyasaji wa kijinsia lakini pia kuondokana na madhira na madhara ambayo yamekuwa yakiwakabili kwa mingi.
Hayo yamesemwa leo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw. Richard Kwitega wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha wadau wa sera ya jinsia kanda ya kaskazini kwa lengo la kujadili na kutoa maoni katika mchakato unaoendelea wa kuifanyia marekebisho sera ya Taifa ya Jinsia ya mwaka 2000.
Aidha Bw. Kwitega ameongeza kuwa Mkoa wa Arusha ambao wananchi wake wengi ni wafugaji mwanamke amekuwa hapewi kuipaumbele sana katika masuala ya elimu na uchumi hivyo amewataka wanawake kushirikiana na Wizara kuthimi hali ya mambo na kutumia fursa hii kuakikisha masuala yao yanaingizwa katika sera hii.
Bw. Kwitega ameongeza kuwa mpaka hivi sasa wanawake katika Wilaya ya Longido bado walikuwa wakizuiwa kula mayai na kuongeza kuwa wanawake hao watumie fursa hii kuhakikisha masuala ya lishe pia yanaingizwa katika sera hii inayaofanyiwa marekebisho.
Naye Mkurugenzi wa Msaidizi Idara ya Jinsia Bi. Grace Mwangwa amesema kuwa Sera hiyo imekuwepo kwa kipindi cha takribani miaka 19 hivyo kwa sasa ni wakati sahihi kwa Serikali kufanya mapitio ya Sera hiyo na kuifanyia maboresho ili iweze pia kuendana na mabadiliko yaliyopo ya sayansi na teknolojia pamoja na mabadiliko ya sheria zilizopo kuhusu maendeleo ya jinsia Nchini.
Bi. Mwangwa amewataja wadau muhimu katika kuhakikisha Sera hiyo inafanyiwa marekebisho kuwa ni wawakilishi wa wanawake, maafisa ustawi wa jamii, Maafisa Maendeleo ya Jamii, Wadau kutoka Mashirika yasiyo ya Kiserikali pamoja na wawakilishi wa watu wenye mahitaji maalum katika jamii kwa lengo la kuhakikisha hakuna kundi hata moja katika jamii litakalo achwa nyuma katika mababoresho ya sera hiyo.
Bi. Mwangwa ameongeza kuwa mpaka sasa mchakato wa kufanya tathimini na ktoa maoni unaendelea katika kanda saba na kanda hii ya kaskazini ni ya nne katika mfululizo wa utoaji maoni na utegemea kuendelea katika kanda zilizobaki.
Mshauri Mwelekezi wa mapitio ya Sera ya Taifa ya Jinsia Profesa Linda Mhando amesema Tanzania kwasasa imesaini makubaliano mbalimbali ya kimataifa ambayo hayakuwepo wa katika sera ya awali hivyo ni wakati muhafaka wa kufanya mabadiliko katika sera hiyo ambayo amedai imepitwa na wakati hivyo kuifanyia mabadiliko ili iweze kuendana na makubaliano ya kimataifa yaliyoko.
Profesa Mhando ameongeza kuwa katika maoni ambayo yamekuwa yakitolewa imeonekana mwanaume aliachwa nyuma hivyo mabadiliko ya sera hii yatafanya pia sera hii kuzingatia pia jinsia ya kiume kwani mwanaumea akiachwa nyuma uko mbeleni tunaweza kujikuta hatupigi hatua.
Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii inakutana pamoja na wadau Jijijini Dar es Salaam kwa lengo la kufanya mapitio ya Sera ya Jinsia ya Mwaka 2000 pamoja na mkakati wa utekelezaji wake wa mwaka 2005 na kuifanyia tathimini ili iweze kuendana na mabadiliko yaliyopo kwa sasa.

No comments: