ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 6, 2020

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, SULEIMAN MZEE AKUTANA NA WAKUU WA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA, LEO JIJINI DAR

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Suleiman Mzee akifanya mazungumzo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo alipotembelea leo Makao Makuu ya Jeshi ikiwa ni ziara yake maalum ya kujitambulisha kwa Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama tangu aapishwe kuwa Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara, Februari 3, 2020.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Seleman Mzee akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa, Diwani Athumani alipomtembelea ofisini kwake leo mara baada ya mazungumzo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee akisalimiana na Maafisa wa Uhamiaji alipowasili katika Ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji, Jijini Dar es Salaam leo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee (kulia) akiteta jambo na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala (meza kuu) pamoja na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Uhamiaji(hawapo pichani) alipotembelea Makao Makuu ya Uhamiaji, leo jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbungo (kushoto) akimkabidhi Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee baadhi ya vipeperushi mbalimbali vyenye ujumbe wa mapambano dhidi ya rushwa alipotembelea Ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam(Picha zote na Jeshi la Magereza).

No comments: