Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe.
Dar es salaam. Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu imemtaka mdhamini wa Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kujitathimini kwa kuwa ameshindwa kujua mshtakiwa huyo alipo.
Hatua hiyo imekuja baada ya mdhamini huyo,Ray Kimbita kuieleza Mahakama kuwa amepewa taarifa za kuugua kwa Zitto akiwa Marekani wakati akijiandaa kurejea nchini.
Jana, mahakama ilikuwa itoe uamuzi katika kesi ya uchochezi namba 327 ya mwaka 2018 inayomkabili Zitto kama ana kesi ya kujibu au la, baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi kwa kuita mashahidi 15.
Hakimu mkazi mkuu, Huruma Shahidi alieleza kutokana na maelezo ya mdhamini huyo hakuna anayejua Zitto yuko wapi.
“Nakutaka mdhamini ujitathimini kwa kuwa umeshindwa kujua mtuhumiwa alipo,” alieleza Hakimu Shahidi.
Kesi itatajwa Februari 18 na Zitto ametakiwa kuwepo mahakamani siku hiyo
No comments:
Post a Comment