Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu maswali ya wabunge wakati wa Bunge la kumi na nane Jijini Dodoma tarehe 6 Februari 2020.
Sehemu ya mawaziri akiwemo Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb), Waziri wa TAMISEM Mhe Suleima Jaffo na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mhandisi Hamad Masauni wakifatilia kipindi cha maswali na majibu akijibu maswali ya wabunge wakati wa BUnge la kumi na nane Jijini Dodoma tarehe 6 Februari 2020.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu maswali ya wabunge wakati wa Bunge la kumi na nane Jijini Dodoma tarehe 6 Februari 2020.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Serikali inatekeleza Mradi wa Kuendeleza Skimu za Umwagiliaji za Wakulima Wadogo (Small Scale Irrigation Development Project -SSIDP) ikiwa ni pamoja na Skimu ya Umwagiliaji ya Nyida.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) ameyasema hayo Bungeni tarehe 6 Februari 2020 Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe Azza Hilaly Hamad aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itachimba bwawa kwa ajili ya kuboresha Mradi wa Umwagiliaji Nyida?
Mhe Mgumba amesema muwa katika kutekeleza Mradi huo, Kampuni ya Shekemu Construction Ltd inafanya kazi ya ujenzi wa miundombinu kwa ajili ya kuboresha mfumo wa usambazaji maji mashambani ambapo utekelezaji wa Mradi huo kulingana na Mkataba umefikia asilimia 68 ya kazi zote za ujenzi.
Ameongeza kuwa hadi kufikia mwezi Disemba 2019 jumla ya Tsh. 282, 154,880.68 zimelipwa kwa Mkandarasi kati ya Tsh 466,594,981.81 zilizotengwa kwa ajili ya kuendeleza Skimu ya Nyida.
Hata hivyo Mradi huo kwa sasa umesimama kupisha msimu wa kilimo kwa wakulima na mvua zinazoendelea kunyesha. Hivyo, Mkandarasi ataendelea na kazi iliyobakia kulingana na Mkataba mara baada wakulima kuvuna mazao yao na Msimu wa mvua kumalizika.
Mhe Mgumba amesema kuwa kutokana na mabadiliko ya tabianchi na mvua zisizotabirika pamoja na wakulima kuwa na mwamko mkubwa wa kilimo cha umwagiliaji wa kutaka kuongeza uzalishaji, tija kwa kulima misimu miwili kwa mwaka na kwa kuzingatia kuwa chanzo cha maji cha skimu hiyo ni mto Manonga ambao ni wa msimu na hivyo Serikali iliona umuhimu wa ujenzi wa Bwawa ili kuendeleza skimu hiyo.
Aidha, ili kutekeleza mradi huo, mwaka 2013 Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya ya Shinyanga na Nzega zilifanya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa awali kwenye eneo linalokusudiwa kujengwa bwawa la Nyida eneo la Lyamalagwa litalokuwa na uwezo wa kumwagilia maji mita za ujazo 4,167,825 na gharama ya shilingi 3.5 bilioni kwa wakati huo.
Kadhalika, Kutokana na mabadiliko ya kimuundo ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, na miradi mingi ya umwagiliaji kujengwa chini ya kiwango, Serikali haikuweza kutekeleza mradi huo kwa wakati kutokana kufanya tathmini ya kina ya ufanisi ya miradi hiyo na hivyo kushindwa kutekeleza mradi kwa wakati.
Aidha, kwa kuwa muda mrefu umepita tangu tahtmini hiyo ifanyikke, Serikali itafanya mapitio upya ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ili kupata mahitaji na gharama halisi ya ujenzi wa bwawa na athari zake kwa sasa.
No comments:
Post a Comment