Saturday, April 4, 2020

DC MBONEKO AHAMASISHA WAFANYABIASHARA NA WANANCHI KULIPA KODI YA PANGO LA ARDHI SHINYANGA

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) akitoa elimu ya ulipaji kodi ya pango la ardhi kwa Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Phantom Oil Tanzania Ltd John Maguru (kushoto) inayodaiwa shilingi milioni 105 za pango la ardhi tangu mwaka 2007 leo Alhamis Aprili 2,2020 wakati akiongoza Kampeni ya Kuhamasisha Ulipaji wa Kodi ya Pango la Ardhi kwa wamiliki wa viwanja vya Biashara na makazi katika manispaa ya Shinyanga. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Idara ya Ardhi na Mipango Mji Manispaa ya Shinyanga,Salu Ndongo akifuatiwa na Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Denis Masami. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog.
Kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Phantom Oil Tanzania Ltd John Maguru akimuahidi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kuwa Kampuni yao ipo tayari kuanza kulipa kodi ya pango la ardhi.
Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Denis Masami (katikati) akielezea hatua zinazochukuliwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa wafanyabiashara na wananchi wasiolipa kodi ya pango la ardhi kuwa ni pamoja na kuchukua hatua za kisheria kwa kusambaza hati za madai ili kuwafikisha mahakamani watakaokaidi tutawakamata mali na kuuza ili kufidia deni husika.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akipokelewa na Meneja wa Kiwanda cha Machinjio ya Punda cha Fang’ Wah, Alice Mingyang Yan (kulia) alipotembelea kiwanda kicho kwa ajili ya kuhamasisha Ulipaji wa Kodi ya Pango la Ardhi kwa wamiliki kiwanda hicho kilichopo Ibadakuli katika manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikagua nyaraka mbalimbali katika Kiwanda cha Machinjio ya Punda cha Fang’ Wah na kubaini kuwa Kiwanda hicho kinadaiwa shilingi milioni 66 za pango la ardhi tangu mwaka 2013 na kuwataka walipe deni hilo.
Wafanyakazi wa kiwanda cha Kiwanda cha Machinjio ya Punda cha Fang’ Wah wakijitetea mbele ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kuwa wao walinunua kiwanda hicho mwaka 2018 kutoka kwa Mwekezaji Mwingine hivyo wapo tayari kuanza kulipa deni la kuanzia mwaka 2018 hadi 2020.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) akiwataka wamiliki wa kiwanda cha Fang’ Wah kulipa kodi ya pango la ardhi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza na waandishi wa habari katika Kiwanda cha Machinjio ya Punda cha Fang’ Wah na kuhamasisha ulipaji wa kodi ya pango la ardhi.
Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Denis Masami akitoa elimu ya ulipaji kodi ya pango la ardhi kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment Ltd, Gasper Kileo (wa pili kulia) ambaye pia anadaiwa deni la shilingi milioni 120 kwa ajili ya pango la ardhi katika kiwanja chake kilichopo katika eneo la Matanda.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akimhamasisha Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment Ltd, Gasper Kileo kumalizia kulipa kodi ya pango la ardhi anayodaiwa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment Ltd, Gasper Kileo akielezea hatua alizochukua baada ya mgogoro wa ardhi kuisha katika viwanja vyake katika eneo la Matanda ambapo kwa kutambua umuhimu wa kulipa kodi tayari alishaanza kulipa deni analodaiwa.
Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akitoa elimu ya ulipaji kodi ya pango la ardhi kwa Mkurugenzi wa Mwananchi Garage Polycarp Kimario (kulia) ambaye anadaiwa kodi ya shilingi milioni 9.3 katika kiwanja chake ambacho anakitumia kufuga samaki.
Kulia ni Mkurugenzi wa Mwananchi Garage Polycarp Kimario akimuahidi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kuwa atalipa kodi ya pango la ardhi mwezi huu Aprili 2020.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiwahamasisha wamiliki wa ardhi kuhakikisha wanalipa kodi ya pango la ardhi.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko ameongoza Kampeni ya Kuhamasisha Ulipaji wa Kodi ya Pango la Ardhi kwa wamiliki wa viwanja vya biashara na makazi katika manispaa ya Shinyanga inayoendeshwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili kutoa elimu ya ulipaji kodi na kufuatilia wadaiwa wenye madeni makubwa na malimbikizo ya muda mrefu

No comments: