ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 1, 2020

Mjengo wa Beckham huko Miami usipime,corona yamkimbiza hapo,aenda kijijini

Inside the Beckhams' $20m Mediterranean-style waterfront holiday ...
Is David Beckham Bending It Into A Star Island Home? - South ...
MIAMI, MAREKANI . SUPASTAA David Beckham na mkewe mrembo Victoria wameripotiwa kutumia Pauni 20 milioni kwenye makazi yao ya kifahari yaliyopo kwenye ghorofa moja huko Miami.

Jengo huo lilijengwa kama makumbusho huko Miami lilikamilika mwishoni mwa mwaka jana na lina vyumba vitano vya kulala, bwawa la kuogelea na uwanja wa kutua helikopta uliojengwa juu ya paa.

Hayo ni makazi mengine ya kisasa kabisa yanayomilikiwa na staa huyo wa zamani wa Manchester United, Real Madrid na England huku akimiliki pia jumba la maana huko London lenye thamani ya Pauni 31 milioni na makazi mengine yenye thamani ya Pauni 6 milioni huko Cotswolds.

Familia hiyo ya Beckham kwa sasa itatumia muda mwingi zaidi kwenye Jiji la Miami kutokana na kuwa na timu yao mpya ya soka, Inter Miami, inayoshiriki Ligi Kuu Marekani. Taarifa zinadai kwamba Beckham na familia yake walifanya ziara kwenye jengo hilo miezi michache kabla ya kukamilika na hapo wakakubali kuwa miongoni mwa wakazi 84 watakaoishi kwenye ghorofa hilo. Ghorofa hilo ni moja ya majengo marefu yaliyopo kwenye jiji hilo na Beckham amependa eneo hilo kwa sababu linamfanya awe na uwezo mkubwa wa kuitazama vyema Miami. Gharama za kupanga kwenye jengo hilo ni kuanzia Pauni 4.7 milioni hadi Pauni 17.6 milioni.

Ukiweka kando bwawa la kuogelea na uwanja wa helikopta, jengo hilo pia lina vyumba viwili vya huduma ya spa, saluni, baa ya vinywaji laini na eneo la kuota jua.

Jengo hilo lilibuniwa na msanifu majengo, Zaha Hadid (marehemu), ambaye pia ndiye aliyebuni lile jengo la Stratford lililotumika kwenye michezo ya Olimpiki 2012 huko London. Sehemu kubwa ya makazi ya Beckham kwa sasa ni Miami kutokana na kuwa na timu yake kwenye eneo hilo.

Hata hivyo, kwa sasa familia hiyo imejifungia kwenye makazi yao huko Cotswold kwa ajili ya kujiweka mbali na maambukiia ya virusi vya corona.

Watoto wao Brooklyn, Romeo, Cruz na Harper Seven wote wameungana na wazazi wao kwenye makazi hayo ya kijijini.

Beckham alituma ujumbe wake Instagram akisema: “Nataka kuwatakia heri wote waliopo kwenye changamoto ya mapambano ya janga hilo (la corona) lililoikumba dunia. Tutapita kwenye hili pamoja na tuweke mkazo zaidi kwenye kujilinda wenyewe, wapenzi wetu na jamii zetu. Tuwe salama.”

No comments: