Wednesday, April 1, 2020

SISI TUTAJILINDA KUTOKANA UWEZO WETU

Na Mwandishi wetu, Vijimambo Blog
Kauli aliyotoa spika wa Bunge Mhe. Ndugai kwamba sisi hatuwezi kuwaiga wazungu jinsi ya kujikinga na kirusi Corona sidhani kama ilikua kauli sahihi ukizingatia yeye ni kiongozi mkuu wa Bunge na waTanzania wengi wanamfuatilia na kumsiiliza kauli anazotoa kama kiongozi mkuu wa Bunge letu.

Ni vitu gani ambavyo Tanzania haiwezi kuvifuta katika kuhakikisha ugonjwa huu ausambai na kuhatarisha maisha kama ilivyotokea kwa nchi zilizoendelea kama China, Italia na Marekani,

Mambo ambayo wananchi wanatakiwa kufanya
      1. kuepuka na misongano kitu kama hichi hakihitaji pesa kuepukana nacho.
      2. unapoongea na mwenzako kaa nae futi 6, hili nalo halihitaji pesa kufanya hivyo.
      3. kuepuka safari zisizo kuwa za lazima. Kufanya safari ni kuongeza gharama sasa hili lina tatizo           gani kulitimiza kwa usalama wa wananchi wetu.
      4. Kunawa mikono na sababuni mara kwa mara, haya na mengineyo hayahitaji gharama yeyote              zaidi ya matendo yetu kuchukua hatua.
      5. Usiamini unayekutana naye mhesabie anamaambukizi ya corona. Hili limekuta ni tatizo kwa             nchi yetu kwa sababu bado misongamono ni mingi sana watu wakaribiana sana hatuka umbali            wa mtu na mtu, bado watu wanashikana mikono, hili ni tatizo tusipojihadhari nalo litatumaliza           waTanzania.

Nachotaka kuelezea mi kwamba tusifanye masihara na huu ugonjwa tuangalie mifano kwa nchi zilizoendelea ulivyowatafuna mpaka leo wanashindwa kuuthibiti, utakapolipuka huko kwetu tutashindwa pa kukimbilia.

Nchi kama Marekani pamoja na nguvu ilizokua nazo, fedha, mahospitali ya hali ya juu, madaktari na wataalamu mbalimbali wa hali ya juu, pamoja na hayo yote wamezidiwa mpaka leo April 1, 2020 maambukizi ya corona yamefikia 189,815 waliopo hospitali ni 185,737, vifo 4,078 na wanaopona ni 7,136 sasa tujipime na sisi kwa staili hiyo.

pamoja na umaskini tulionao tahadhari inawezekana kwa sababu ugongwa huu utakapolipuka kwa kasi sijui tutakimbilia wapi, naomba viongozi wetu tuwe mstari wa mbele na tuwe mifano kwa watu wetu katika kulinda maisha, uchumi ukianguka ni rahisi kujipanga na kuinua upya lakini uhai wa mtu hauinuliki tena.

No comments: