ALIYEKUWA kuwa waziri wa mambo ya nje, Bernard Membe, leo Julai 19, 2020, amerejesha fomu za kuomba kuteuliwa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya ACT Wazalendo.
Makabidhiano hayo yamefanyika Ofisi ya ACT Wazalendo Magomeni, jijini Dar es Salaam ambapo amekabidhi fomu hizo kwa Naibu Katibu Mkuu Bara wa ACT Wazalendo, Joran Bashange.
Membe ambaye alitaja kauli-mbiu yake kuwa ni Kazi na Bata, alikubali kuwania nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo, kwa alichodai kwamba ni wakati muafaka kwake kushiriki mazungumzo na vyama vingine ili waweze kusimamisha mgombea mmoja. GPL
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake