Nchi zilizoshiriki katika mkutano huo uliofanyika kwa njia ya mtandao yaani virtual meeting ni pamoja na Ivory Coast,Misri,Djibout,Rwanda,Burikanafaso pamoja na Tanzania kwa lengo la kujadiliana namna ya kupambana na uhalifu wa kimataifa kutokana na baadhi ya wahalifu kutumia mwanya wa uwepo wa ugonjwa wa COVID 19 kutekeleza uhalifu ikiwa ni pamoja na usafirishaji wa dawa za kulevya,uuzaji wa dawa na vitenganishi bandia kwa ajili ya ugonjwa huo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi ameongeza kuwa kauli mbiu ya mkutano huo ni “huwezi kupiga makofi kwa mkono mmoja” ikiwa na maana ya kuzitaka nchi mbalimbali duniani kushirikiana kwa lengo la kupambana na uhalifu wakati huu wa corona kwa kubadilishana uzoefu kutokana na wahalifu kubadili mbinu.
Aidha Prof. kabudi ameitumia fursa hiyo kuelezea hatua ambazo Tanzania imezichukua kupitia jumuiya za kikanda ikiwemo na Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC ambayo kwa sasa Tanzania ni Mwenyekiti wake
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake