ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, July 14, 2020

RAIS WA ZANZIBAR ALHAJJ DK. SHEIN AMEJUMUIKA NA WAUMINI WA DINI YA KIISLAM KATIKA KISOMO CHA HITMA YA MAREHEMU NYANYA D

WAUMINI wa Dini ya Kiislam wakishiriki katika kisomo cha hitma kumuombea dua Marehemu Haji Nassib Haji Nyanya kilichofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Chuwini Wilaya ya Magharibi “A” Unguja.(Picha na Ikulu) WAUMINI wa Dini ya Kiislam wakiitikia dua ya kumuombea Marehemu Haji Nassib Haji Nyanya iliofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Chuwini Wilaya ya Magharibi “A” Unguja, ikisomwa na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Hassan Othman Ngwali (hayupo pichani) (Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj .Dk. Ali Mohamed Shein akiitikia dua ya kuhitimisha kisomo cha hitma ikisomwa na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Hassan Othman Ngwali (kushoto kwa Rais) na (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, dua hiyo imefanyika katika Msikiti wa Ijumaa Chuwini Wilaya ya Magharibi “A” Unguja.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj .Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na kuagana na Waumini wa Dini ya Kiislam baada ya kumalizika kwa kisoma cha dua kumuombea Marehemu Haji Nassib Haji Nyanya, kilichofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Chuwini Wilaya ya Magharibi “A” Unguja.(Picha na Ikulu)RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj. Dk. Ali Mohamed Shein akijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam katika kisomo cha Hitma kumuombea Dua Marehemu Haji Nassib Haji Nyanya na (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na (kushoto kwa Rais) Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Hassan Othman Ngwali, kisomo hicho kimefanyika katika msikiti wa Ijumaa chuwini Wilaya ya Magharibi “A” Unguja.(Picha na Ikulu)

No comments: