Tuesday, July 21, 2020

UJENZI WA VIVUKO BUGOROLA UKARA, CHATO NKOME KUKAMILIKA AGOSTI

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle wa pili kushoto akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala huo Prof. Idrissa Mshoro wa pili kulia wakati wakikagua maendeleo ya ujenzi wa vivuko vya Bugorola Ukara na Chato Nkome katika tukio lilofanyika katika yadi ya Songoro. Ujenzi wa vivuko hivyo unategemewa kukamilika ifikapo mwezi Agosti mwaka huu, ujenzi huo umechelewa kukamilika kama ilivopangwa kutokana na kutokea kwa ugonjwa wa mafua makali maarufu Covid 19. Kulia ni meneja wa TEMESA Mwanza Mhandisi Hassan Karonda na kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni ya Songoro inayojenga vivuko hivyo Major Songoro.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle akisoma taarifa ya ujenzi na ukarabati wa karakana ya TEMESA mkoa wa Mwanza wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala huo Prof. Idrissa Mshoro wa pili kulia katika tukio lililofanyika katika karakana hiyo. Kushoto ni meneja wa TEMESA Mwanza Mhandisi Hassan Karonda na kulia ni mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Mwanza Mtakwimu Bi. Suzan Ndunguru. Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle aliyenyoosha mkono akimuonyesha maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa majengo mapya ya karakana ya mkoa wa Mwanza Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala huo Prof. Idrissa Mshoro wa pili kulia wakati alipotembelea karakana hiyo kujionea ujenzi unavyoendelea. Kulia ni meneja wa TEMESA Mwanza Mhandisi Hassan Karonda.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle kulia akimueleza jambo Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala huo Prof. Idrissa Mshoro wa pili kulia wakati alipotembelea karakana hiyo kujionea maendeleo ya ujenzi na ukarabati wa karakana hiyo unavyoendelea. Wa tatu kulia ni meneja wa TEMESA Mwanza Mhandisi Hassan Karonda.
Muonekano wa kivuko ambacho kitatoa huduma kati ya Bugorola na Ukara ambacho kinaendelea kujengwa katika yadi ya Songoro iliyopo Ilemela, kivuko hicho pamoja na vivuko vya Mafia na Nyamisati na Chato Nkome vinatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Agosti mwaka huu.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle kushoto, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala huo Prof. Idrissa Mshoro katikati na Mkurugenzi wa kampuni ya Songoro Major Songoro wakipita pembeni ya kivuko kinachotarajiwa kutoa huduma kati ya Bugorola na Ukara wakati walipokua wakikagua maendeleo ya ujenzi wa vivuko ambavyo vinatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Agosti mwaka huu. Tukio hilo lilifanyika katikayadi ya Songoro iliyopo Ilemela.

PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA MWANZA)

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake