Tuesday, July 28, 2020

UWANJA WA MICHEZO TAIFA WABADILISHWA JINA SASA BENJAMIN WILLIAM MKAPA STADIUM

Na Shamimu Nyaki – WHUSM
Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ametangaza rasmi
kuwa kuanzia leo Julai 29, 2020 Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam utaitwa Uwanja wa
Uwanja wa Benjamin Mkapa (Benjamin Mkapa Stadium) ili kuendelea kumuenzi Rais huyo wa
awamu ya Tatu.

Rais Magufuli ametoa tamko hilo katika hafla ya kuaga mwili wa aliyekuwa rais wa serikali ya
awamu ya tatu Hayati Benjamin William Mkapa iliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru
Dar es Salaam ambapo alisisitiza Mzee Mkapa alikuwa na mchango mkubwa katika sekta ya
michezo nchini hivyo taifa tunapaswa kumuenzi .

“Mzee Mkapa aliujenga uwanja mkubwa wa michezo na alikua hapendi vitu viitwe kwa jina
lake,lakini kwakuwa kwa sasa amelala na hawezi kuniadhibu na kwakua nimepokea meseji
nyingi nimekubali na sasa natamka rasmi uwanja ule uitwe Mkapa Stadium,”Dkt.Magufuli.

Dkt.Magufuli ameongeza katika Michezo Mzee Mkapa alikuwa anapenda sana michezo ndio
maana amefanya mambo mengi sana katika sekta hiyo,vile vile alikua ni Shabiki wa Timu ya
Yanga japo hakuwahi kuonyesha hadharani hivyo tunapaswa kumkumbuka na kutunza
kumbukumbu hizo.

Hata hivyo Uwanja wa Taifa Dar es Salaam (Mkapa Stadium) ni miongoni mwa viwanja
vikubwa barani Afrika ambavyo vimekidhi vigezo vyote vilivyoanishwa na Shirikisho la
Soka Duniani FIFA na una uwezo wa kuingiza mmashabiki takriban elfu sitini.

Hivi karibuni watu wengi walionyesha nia yao ya kuomba uwanja huo uitwe jina la
Mzee Mkapa kama njia ya kumuenzi Rais huyo mstaafu ambayo leo Mhe.Rais
ameitimiza nia hiyo.

Pamoja Mheshimiwa Rais Magufuli aliendelea kusisitiza kuwa Mzee Mkapa katika sekta ya Sanaa
napo ameacha alama kwani ndiye aliyeanzisha Chama cha Hakimiliki na Hakishiriki (COSOTA)
ambayo kwa sasa ni taasisi rasmi lengo ni kuwasaidia wasanii kupata haki za kazi zao na
katika sekta ya Habari ndiye muasisi wa Vitengo vya Habari na Mawasiliano katika wizara.

Naye mmoja wa wananchi na shabiki wa mpira nchini Bw.Athuman Ugassa amepongeza uamuzi
Mheshimiwa Rais Magufuli wa kuupa uwanja huo jina lake kwani uwanja huo ni alama ya
mchango wake katika kuendeleza sekta ya michezo nchini.

 


No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake