Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, marehemu Benjamin William Mkapa ambako walikwenda kutoa pole kwa familia, Julai 24, 2020. Picha kwa hisani ya GPL
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa, nyumbani kwa marehemu , Masaki jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin Mkapa utaagwa kwa siku tatu mfululizo kuanzia Julai 26-28 Jijini Dar es Salaam, na utazikwa siku ya Jumatano katika Kijiji cha Lupaso, Masasi mkoani Mtwara.
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima nae miongoni mwa waombolezaji waliofika kwenye Msiba nyumbani kwa aliyekuwa raisi wa awamu ya tatu Benjamin William Mkapa hapa Masaki Jijini Dar es Salaam kutoa mkono pole kwa familia.
Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira, Mussa Zungu ameungana na viongozi mbali mbali nyumbani kwa Marehemu Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania, Benjamin William Mkapa kutoa mkono wa pole kwa familia, ndugu, jamaa na Watanzania nyukbani kwa marehemu, Masaki jijini Dar es salaam.
“Tunamengi ya kujifunza kwa wazee wetu, tuna kila sababu ya kuwaenzi kwa matendo, kijana yeyote aliyekuwepo kwenye nafasi na aliye na ndoto, ajue kwamba Benjamin Mkapa ni moja ya nguzo katika taifa hili” -Paul Makonda – Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa DSM.
Waziri wa Mambo ya Nje Prof. Paramagamba Kabudi akisaini kitabu cha Maombolezo nyumbani kwa Hayati Rais wa Awamu ya tatu wa Tanzania Mh. Benjamin Mkapa aliyefariki leo hii Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi amewasili nyumbani kwa Marehemu Rais wa Awamu ya tatu wa Tanzania Benjamin William Mkapa akijumuika na viongozi mbali mbali pamoja na waombolezaji kuomboleza kifo cha kiongozi huyo.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake