Mheshimiwa Majaliwa akizungumza
na Mianga hospitalini hapo. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa
MOI Dkt. Respicious Boniface, (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana
(Ijumaa Julai 24, 2020) alimjulia hali kijana Deogratias Mianga mkazi wa
Singida ambaye amelazwa katika Taasisi ya tiba ya Mifupa Muhimbili
(MOI) kwa ajili ya matibabu.
Waziri Mkuu alimuona Deogratias
kupitia vyombo vya habari akiomba msaada wa matibabu kutokana na
matatizo ya mgongo. Waziri Mkuu aliguswa na hali ya Deogratius na
tarehe 02/07/2020 alimuwezesha kufika MOI na kufanyiwa upasuaji tarehe
06/07/2020.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake