Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji Angela Kairuki akisalimiana na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi -Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Abel Mtui alipowasili katika hifadhi hiyo kukagua shughuli za uwekezaji ,katikati ni Kamishna manadamizi wa Uhifadhi Kanda ya Kaskazini ,Herman Batiho.
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji Angela Kairuki akiwa ameongozana na Mkuu wa wilaya ya Same ,Rosemery Senyamule na Makamishna wa uhifadhi wakielekea katika eneo ambalo kumefanyika uwekezaji wa nyumba za wageni wanaofika kwa ajili ya shughuli za utalii katika hifadhi ya taifa ya Mkoamazi.
Moja ya Nyumba zilizojengwa katika eneo la Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi kwa ajili ya malazi kwa wageni wanaofika katika hifadhi hiyo.
Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi wa Kanda ya Kaskazini Herman Batiho akimjeleza jambo Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji Angela Kairuki baada ya kutembelea sehemu ya uwekezaji wa nyumba kwa ajili ya malazi kwa wageni wanaofika katika hifadhi hiyo.
Kamishanna Msaidizi wa Uhifadhi aliyekuwa Mkuu wa Hifadhi ya taifa ya Mkomazi ,kabla ya kuhamishiwa Uduzungwa Abel Mtui akitoa maelezo kwa Waziri Kairuki kuhusu maeneo ya uwekezaji yaliyoainishwa katika Hifadhi hiyo.
Mkuu mpya wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi ,Kamishna Msaidizi Emanuel Moirana akitambulishwa wakati wa ugeni huo.
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu -Uwekezaji Angela Kairuki akizungumza mara baada ya kutembelea sehemu ya uwekezaji uliofanyika katika hifadhi ya taifa ya Mkomazi.
Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi Kanda ya Kaskazini ,Herman Batiho akikabidhi zawadi ya vikombe vyenye nembo ya TANAPA kwa Waziri Kairuki.
Na Dixon Busagaga ,Same.
Waziri wa Nchi ofisi
ya Waziri Mkuu –Uwekezaji Angela Kairuki ameliomba Shirika la Hifadhi za Taifa
(Tanapa) kuipa upendeleo maalumu Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi kama zilivyo
hifadhi za Kusini na Magharibi badala ya kuiweka katika kundi la hifadhi za
Kaskazini zinazo weza kujitegemea.
Kairuki ametoa ombi
hilo wakati wa ziara yake aliyofanya katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi
kuangalia uwekezaji wa eneo la maladhi kwa ajili ya wageni kutoka ndani na nje ya
nchi wanaofika kwa ajili ya kutembelea hifadhi hiyo.
Akizungumza mara baada
ya kukagua nyumba zilizotengwa kwa ajili ya malazi katika hifadhi hiyo Waziri Kairuki alisema kama wasimamizi wa eneo
la uwekezaji, wataendelea kutafuta wawekezaji kwa ajili ya kuwekeza miundombinu
ya majengo katika hifadhi hiyo,.
“Mmeniambia mna maeneo
(Site)karibia Saba,na Tano zimeshapata wawekezaji, bado mbili, tutaendelea
kushirikiana pamoja kutafuta wawekezaji ambao watakuja kuwekeza katika maeneo
hayo,Rai yangu kwenu, mmeanza na hiki kidogo, ila mna uwezo wa kuweka
miundombinu ya jengo”alisema Kairuki.
“Fedha mnazo,mnaweza
kuwekeza kwenye Jengo la malazi ya kutosha kwa vigezo mlivyovisema, na
ninafahamu kuendesha wenyewe si kazi nyepesi, ila mnaweza kujenga miundombinu
na kisha kutafuta watu wa kuiendesha kama mameneja”.
Alisema “Pamoja na
kwamba na sisi tutatafuta wawekezaji wengine, lakini Rai yangu ni kwamba na
ninyi,muonyeshe uwekezaji mmoja, halafu mtafute waendeshaji au mameneja, maana
duniani unaposikia, mahoteli makubwa yakitajwa,kama Serena, waliojenga si
wamiliki, wengine wameweka uwekezaji,halafu wanaokuja kuweka uwekezaji ni mtu
mwingine, hivyo nanyi Tanapa mnaweza kufanya hivyo hapa Mkomazi”
Aidha Kairuki alitumia
pia nafasi hiyo, kuitaka Hifadhi ya Mkomazi, kutengeneza kitabu kidogo,
kitakachoelezea ndege waliopo katika hifadji hiyo na tabia zake kwa maelezo ya
kitaalamu kwa lugha nyepesi,ili watu watakaofika waweze kuwafahamu ndege hao
kwa undani.
“Numeambiwa hapa
Mkomazi,kuna aina 450 za ndege,sasa nishauri,tengenezeni kitabu kidogo kizuri
kinachovutia, kitakachokuwa kinaelezea ndege wote waliopo katika hifadhi
hii,tabia zao na maelezo ya kitaalamu kwa lugha nyepesi,ili watu watakaokuja
kutembelea, wafahamu anamuona ndege yupi na ni wa aina gani”
Akizungumza Mkuu wa
Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule, alisema hifadhi ya Mkomazi bado inahitaji
kutangazwa na kuomba kutafutiwa wawekezaji ambao watawekeza hoteli za hadhi
mbalimbali ndani ya Hifadhi na hata Wilaya ya Same, ili kuvutia wageni
mbalimbali.
“Mkomazi fursa
ziko nyingi, na inawezekana baada ya mradi huu kuanza, wageni wakawa
wengi,lakini wapo wageni ambao wanaweza kuja tukawapoteza, kutokana na kukosa
hoteli ndani ya hifadhi au Same,hivyo tunaomba tupate wawekezaji wa kuwekeza
hapa, hata hoteli za hadhi ya Nyota Tano, maana hifadhi hii inaendelea
kukua”alisema Senyamule.
Naye Kamisha
mwandamizi wa uhifadhi Kanda ya Kaskazini, Herman Batiho, alisema katika
hifadhi hiyo, pamoja na uwepo wa wanyama mbalimbali, pia kuna aina 450 za ndege
wa aina mbalimbali ambao pia wamekuwa kivutio kikubwa cha watalii katika
hifadhi hiyo.
Hifadhi ya taifa ya
Mkomazi inayopatikana kwenye wilaya mbili za Mikoa ya Kilimanjaro na Tanga nikiwa na maana ya Same na Lushoto ni hifadhi
iliyoanzishwa mwaka 1951 kama pori la akiba lililotengwa kutoka Pori kubwa la
Akiba la Ruvu.
Kwa sasa hifadhi hii
ni miongoni mwa hifadhi za Taifa 22 zilizo chini ya Shirika la Hifadhi zaTaifa
(TANAPA) huku maboresho mbalimbali yakiendelea kufanyika katika hifadhi hii ili
kuwavutia wageni wengi zaidi vikiwemo vivutio na miundombinu .
No comments:
Post a Comment