Mkuu wa Gereza la Wilay ya Magu, Mrakibu wa Magereza, Kyelu Bayinga (aliyesinama) akishikiri na maofisa pamoja na askari kupokea msaada wa mbuzi wanyama wawili, mchele kilo 100 na fedha kwa ajili ya kununua sbauni na king’amuzi, kutoka kwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Salum Kalli (wa tano) kutoka kulia.
Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Magu, Mrakibu wa Magereza, Kyelu Bayinga akiwatambulisha mofisa na askari kwa Mkuu wa Wilaya hiyo Salum Kalli baada ya kuzuru gerezani hapo kuzungumza maofisa hao, askari pamoja na wafungwa na mahabusu
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum Kalli, akizungumza na maofisa na askari wa Gereza la Wilaya ya Magu .
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum Kalli, akizungumza na maofisa na askari wa Gereza la Wilaya ya Magu jana baada ya kukagua eneo la mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya askari.
Moja ya nyumba za makazi ya maofisa na askari wa Jeshi la Magereza wilayani Magu ambazo zilijengwa kwa matofali ya tope kama zinavyoonekana kwa sasa hali iliyosababisha wabuni mradi wa kujenga nyumba mpya ili kuboresha makazi yao.
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum Kalli, akikagu bustani ya mboga mboga ya Gereza la Wilaya hiyo jana.Nyuma yake ni Mkuu wa Gereza la Magu, Mrakibu wa Magereza, Kyelu Bayinga.Picha zote na Baltazar Mashaka
NA BALTAZAR MASHAKA, Magu
Mkuu wa Wilaya Magu, Salum Kalli ameahidi kuunga mkono ujenzi wa nyumba 62 za maofisa na askari wa gereza la wilaya hiyo pamoja na zahanati moja zinazojengwa kwa nguvu zao na mapato ya ndani ya gereza hilo.
Alitoa kauli hiyo jana alipozungumza na maofisa pamoja na askari wa gereza hilo akisema kuwa ameguswa na juhudi zao za kutekeleza miradi ya maendeleo ya kujenga nyumba za makazi yao na zahanati kwa nguvu zao hivyo anawatia shime waikamilishe.
Kalli alisema yapo makubwa wameamua kuyafanya na baada ya kuyaona atazungumza na uongozi wa halmashauri kuona namna ya kuwaunga mkono kwa kuezeka jengo la zahanati liweze kuwahudumia askari na jamii ya watu wa Magu.
“Serikali ya Wilaya ya Magu baada ya ninyi (askari)kujenga nyumba hizo tutawaunga mkono kwa kuwatafutia saruji mifuko 100 pamoja na kuezeka ili askari waishi kwenye mazingira na makazi bora wamsaidie Rais Magufuli kuwarekebisha wakosaji (wafungwa) wawe na nidhamu ili wamaliza adhabu zao warudi kuishi na jamii kwa amani,”alisema.
Aidha mkuu huyo wa wilaya alitoa kwa wafungwa na mahabusu wa Gereza la Magu, mbuzi wawili wa kitoweo, mchele kilo 100, sabuni katoni moja, king’amuzi kimoja kiwawezeshe kusikiliza taarifa ya habari na michezo.
“Wafungwa na mahabusu hawa ni Watanzania ni wana jamii, leo wameingia hapa kwa makosa ya wazi au njia nyingine, kesho itakuwa ni sisi .Japo wameikosea jamii, bado tunawapenda na baada ya kumaliza adhabu zao watakuwa wamejirekebisha ili wakirudi wasirejee kutenda makosa kwenye jamii,”alisema Kalli.
Aliwataka maofisa na askari wa gereza hilo kuendelea kuchapa kazi ya kuwahudumia wananchi waihi nao kwa ukarimu na upendo ambapo aliwaahidi kutatua changamoto na baadhi ya mahitaji yao kwenye miradi wanayolenga kutekeleza.
Mkuu wa Gereza hilo Mrakibu wa Magereza, Kyelu Bayinga akitoa taarifa kwa Mkuu wa Wilaya ya Magu, baada ya kutembelea gereza hilo ili kujua kero na changamoto za mahabusu na wafungwa gerezani hapo alisema wanajenga nyumba 62 na tayari wamechimba misingi minane kati ya nyumba 10 za mwanzo kwa gharama ya sh. milioni 300.
Pia alisema gereza hilo linaendesha miradi ufyatuaji wa matofali, ufugaji wa kuku, kilimo cha mazao ya chakula, biashara na mboga mboga zikiwa ni jitihada za kuitikia kwa vitendo agizo la Rais John Magufuli la kuyataka majeshi likiwemo la Magereza kuanza kujitegemea kwa chakula.
Bayinga alisema ujenzi wa nyumba hizo zilenga kuboresha makazi ya askari na maofisa ambapo tayari wanayo mataofari 4,265 ya ujenzi huo na mara baada ya nyumba hizo kukamilika zitawawezesha kuishi kwnye makazi bora ambpo nyumba za zamani zilizojengwa kwa tope zitavunjwa.
“Wafungwa licha ya kutumikia adhabu zao kwa mujibu wa sheria wanazalisha mazao ya biashara (pamba na lozana) na chakula (mihogo, viazi, mtama na mpunga)kwa matumizi yao ambapo zaida wanaua Pia mbali na makazi tunajenga zahanati itakayohudumia askari, jamii, wafungwa na mahabusu wenye changamoto za kiafya,”alisemai Mkuu wa Gereza La Magu.
Awali alieleza mbali na miradi ya kujenga zahanati na nyumba za watumishi, wanahitaji kujenga ukumbi wa burudani ambao wataukodisha (Bwalo na kantini), mradi wa ushonaji wa sare za wafungwa na mavazi ya raia, mashine kwa ajili karakana ya kuchomelea vyuma, vitanda na madirisha,mashine ya kufyatua matofali .
No comments:
Post a Comment