MGOMBEA urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, amekabidhiwa fomu za kuwania urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumatano 28 Oktoba 2020, na Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) jijini Dodoma.
Lissu na mgombea wake mwenza, Salum Mwalimu, wamekabidhiwa fomu hizo leo Jumamosi tarehe 8 Agosti 2020 na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu, Semistocles Kaijage.
Kabla ya kukabidhi fomu hizo, Jaji Kaijage amesema, siku ya uteuzi ni tarehe 25 Agosti, 2020 na siku hiyo wagombea watakuwa na fursa ya kuwasilisha fomu hizo.
Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Charles Mahera, amesema kuna suala la kutafuta wadhamini katika mikoa 10 kat
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake