Tuesday, August 4, 2020

NAIBU WAZIRI SIMA ATOA MIEZI MITATU KUJENGWA MTAMBO WA KUCHAKATA MAJI MACHAFU KATIKA KIWANDA CHA KEDS KIBAHA

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira  Mhe. Mussa Ramadhani Sima amefanya ziara katika kiwanda cha Keds Tanzania Company ltd kilichopo wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani, ili kujionea namna wanavyohifadhi mazingira wakati wa uzarishaji wake.

Katika ziara hiyo Mhe. Sima aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe. Martin Ntemo , Meneja wa NEMC kanda ya Mashariki Bw. Arnold Mapinduzi  pamoja na kikosi kazi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani na NEMC.

Aidha Mhe. Sima ameeleza kuwa kiwanda cha keds kinatakiwa kiwe na mtambo wa kuchakata maji machafu yanayotoka kiwandani kabla ya kurusu kwenda kwenye miundombinu iliyojegwa na serikali na kusambaa ardhini.

“wamiliki wa kiwanda cha keds wahakikishe wanatunza Mazingira hasa kweye suala la maji taka na kemikali zote zinazotoka kiwandani, wahakikishe wanakibali cha kumwaga maji taka kwenye miundombinu iliyojengwa na serikali. Vile vile wajenge mtambo maalum wa kutibu majitaka ili yasiharibu mazigira yetu hii itakuwa ni njia nzuri ya kutunza mazingira na wananchi wetu hawataweza kulalamika” alisema Sima

hata hivyo Mhe. Sima ametoa miezi mitatu kwa kiwada hicho kuhakikisha wameweka mtambo wa kutibu maji machafu yenye kemikali yanayotoka kiwadani “wataalamu wa NEMC walito maelekezo awali waache kumwaga maji machafu yenyekemikali bila kuwepo na utaratibu, sasa wahakikishe wanafata maelekezo yote waliyopewa na wataalamu wa NEMC na waachekutililisha maji machafu hovyo ambayo yanalalamikiwa na wananchi kwenye maeneo yanayozunguka kiwanda hicho. Natoa miezi mitatu waakikishe mtambo huo umejengwa”

Kwaupande wake Bw. Faustine Luhende afisa Afya na Usalama wa Kiwanda cha Keds ameeleza kuwa kiwanda kipo kweye mchakato wa kujega mtambo huo na waliomba wapewe miezi miwili watakuwa wamekamilisha lakini wanamshukuru Mhe. Sima kuwaongezea mwezi mmoja

Aidha Mhe. Sima ametoa pogezi katika kiwada cha lake steel & allied product ltd kilichopo kibaha kwa kufanyauzarishaji wake bila kiharibu Mazingira “nimefika kiwadani hapa nimejionea namna mnavyotunza Mazigira vizuri, nawapongeza kwa hili kwani viwanda vingi vinavyozalisha nondo nchini vimekuwa na changamoto nyingi katika kudhibiti kelele na moshi lakini kweye kiwanda hiki kimeweza kudhibiti chagamoto hizo”.

Hata hivyo akiwa kweye ziara hiyo mhe. Sima alikagua kiwada cha Chisai Innovation Center kinachojishughulisha na uchomaji wa taka hatarishi zinazotoka hospitalini. Alikagua kiwada hicho ili kujionea namna kinavyofanya kazi zake bila kuharibu Mazingira. Aidha ametoa maelekezo kwa Taasisi husika kusimamia shughuli hizi zinaenda ipasavyo ili kuepuka uchafu wa mazigira na kuepusha malalamiko kutoka kwa wananchi.


No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake