ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 12, 2020

Uchaguzi Marekani 2020: Joe Biden amchagua Kamala Harris kuwa Makamu wake iwapo atashinda uchaguzi

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Bw Biden akimfahamisha Bi Harris kwamba atakua mgombea mwenzake siku ya Jumanne

Na BBC
Mgombea wa urais wa chama cha Democratic Joe Biden amemtaja Seneta Kamala Harris kama mgombea mwenza-akiwa ni mwanamke wa kwanza Mmarekani mweusi kugombea wadhifa huo.

Kamala ambaye wakati mmoja alikua hasimu wake katika mchuano wa kuwania urais, ni seneta wa California mwenye asili ya India-na Jamaica ambaye kwa muda mrefu amekua akichukuliwa kama mgombea wa nafasi ya pili baada ya Biden.

Mwanasheria huyo mkuu wa zamani wa California amekua akitoa wito wa kufanyika kwa mageuzi katika polisi ya Marekani wakati wa maandamano ya kitaifa ya kupinga ubaguzi wa rangi

Bwana Biden atakabiliana na Rais Donald Trump katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 3 Novemba mwaka huu.

Bi Harris anasema wakati wote amekuwa akijivunia utambulisho wake na anajieleza binafsi kama ''Mmarekani".

Mwaka 2019, aliliambia jarida la Washington Post kwamba wanasiasa hawapaswi kupewa nafasi etu kwasababu ya rangi au wanakotoka.'' Nilikua nataka kusema hivi: Mimi ni mimi niliovyo. Nina uwezo . Unaweza kuhitaji kunielewa, lakini niko sawa na jinsi nilivyo ," alisema.

Katika mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House Jumanne, Bwana Trump , ambaye ni Mrepuplican , alimuelezea Bi Harris kama '' Mtu ambaye wa kwanza ninayeweza kumchukua''

Bi Harris atakua na mjadahalo na mgombea mwenza wa Trump, Mkamu wa rais Mike Pence, tarehe 7 Oktoba Salt Lake City, Utah.

Ni wanawake wengine wawili tu ambao wamewahi kugombea wa viti vya Makamu wa Rais nchini Marekani -Sarah Palin kutoka chama cha Republican mwaka 2008 na Geraldine Ferraro wa Democrats mwaka 1984. Hatahivyo hakuna mmoja wao aliyeweza kufika White House.

Mwnamke mwenye asili nyeusi hajawahi kuteuliwa kwa tiketi ya urais na vyama vyote viwili. Pia hakuna mwanamke aliyewahi kushinda kiti cha urais nchini Marekani Biden na Harris wamesema nini?

Bwana Biden alituma tweet akisema kwamba amekua na "heshima kubwa" kumtaja Bi Harris kama mtu wake nambari mbili.

Biden na Harris wamesema nini?

Alimuelezea kama "mpiganaji asiye na uoga kwa mwanaume mdogo, na mmoja wa wahudumu bora wa umma ".

Alielezea jinsi alivyofanya kazi karibu na marekemu mtoto wake wa kiume, Beau, alipokua Mwanasheria Mkuu wa California.

"Nilishuhudia walipochukua benki kubwa , wakawainua wafanyakazi, wakawalinda wanawake na watoto dhidi ya unyanyasaji ," he tweeted.

"Nilijjivunia sana wakati huo, najivunia sasa kuwa nae kama mwenzangu katika kampeni hii ."

Baadae Bi Harris alitweet Bwana Biden "anaweza kuunganisha watu wa Marekanikwasababu ameishi miaka yake akipipambana kwa ajili yetu . Na kama rais, atajenga Marekani inayotufaa.

"Nina heshima kujiunga nae kama mtu aliyeteuliwa na chama kugombea kiti cha Makamu wa Rais na kufanya yapasayo kumfanya awe Amir jeshi ."

Kampeni ya Chama ilitangaza kuwa Bwana Biden na Bi Harris watatoa hotuba zao katika Wilmington, Delaware, Jumatano juu ya "jinsi watakavyofanya kazi kwa pamoja kurejesha moyo ya taifa na kupigania familia zinazofanya kazi kuendeleza mbele taifa ".

Bwana Biden aliahidi mwezi Machi kwamba atamtaja mwanamke kugombea wadhifa wa Makamu wa rais. Alikabiliwa na miito mingi kumteua mwanamke mweusi katika miezi ya hivi karibuni wakati taifa lilipokua likikumbwa na maandamano ya kijamii juu ya ukatili wa polisi dhidi ya Wamarekani weusi.

Kamala Harris ni nani?


Bi Harris mwenye umri wa miaka 55, aliondoka kwenye kinyang'anyiro cha kuwania urais mwezi Disemaba baada ya kutofanikiwa kushinda katika mchuano wa uteuzi wa kiti cha urais wa chama cha Democratic.

Akikabiliana mara kwa mara na Bwana Biden wakati wa midahalo ya chaguzi za awali , ambapo alikosoa jinsi Biden alivyosifu mahusiano ya ''kiraia'' ya kikazi aliyokuwa nayo na seneta wa zamani ambaye alipendelea ubaguzi wa rangi.

Alizaliwa katika Oakland, California, na wazazi wahamiaji :Mamayake alikua ni muhindi na baba yake Mjamaica.

Alisoma hadi Chuo Kikuu cha Howard , ambacho ni moja ya vyuo maarufu walivyosomea watu weusi kihistoria. Alielezea muda wake chuoni k= hapo kama moja ya maeneo yaliyojenga maisha yake.

UCHAMBUZI

Wakati mwingine uteuzi unaotarajiwa ni kwa ajili ya sababu inayotarajiwa . Kamala Harris alikua wa mstari wa mbele katika wagombea wa Makamu wa rais hususan tangu wakati ulipotangazwa uteuzi wa Democratic mwezi Machi ambapo Biden alitangaza kuwa atamteua mwanamke kwa tiketi ya mgombea mwenza.

Ni mdogo kwa umri na mwenye nguvu za kuzungumza katika televisheni, na kama binti wa Hamiaji Mjamaica na Muhindi anawakilisha kuongezeka kwa utoaji wa fursa kwa watu wa jamii mbali mbali katika chama cha Democratic.

Zaidi ya hayo, anafahamika kupitia vyombo vya habari, kwa kampeni zake za kuwania urais mwaka 2019 na kwa muda katikakati ya mwaka jana baadhi ya kura za maoni zilimuweka katika nafasi ya kwanza. Wengi miongoni mwa mahasimu wake katika kuwania kiti cha Makamu wa rais hawakufikia kiwango cha kuchunguzwa cha aina hiyo, kwahiyo hapakua na ushahidi kwamba wangeweza kuhimili wadhifa huo.

Faida nyingine aliyokuwa nayo ambayo inapuuzwa kumuhusu Bi Harris ni urafiki aliokuwa nao na Marehemu mtoto wa kiume wa Bwana Biden, Beau, ulioanzishwa wakati wote walipokua wanasheria wakuu. Bwana Biden anathamini sana familia -na uhusiano huo huenda ulimrahisishia kumchagua.

Sasa Bi Harris atakuwa na fursa ya kuanza kampeni tena na kuthibitisha kuwa anastahili uteuzi huu wa kihistoria. Kama atafanikiwa , atakua katika nafasi nzuri ya kutafuta kiti cha urais tena, labda hata mwaka 2024. Leo ameimarisha mizizi yake katika chama cha Demokratic kwa miaka ijayo.

No comments: