UTATA umeibuka baada ya bosi wa Lebo ya Konde Gang Music Worldwide, mwanamuziki Rajab Abdul ‘Harmonize’ au ‘Harmo’ kumtangaza msanii mpya wa lebo hiyo, Raoul John Njeng-Njeng ‘Skales’ kutoka nchini Mwishoni mwa wiki iliyopita, Harmo alitangaza kumsaini msanii wake mpya, Skales baada ya Ibrahim Abdallah ‘Ibraah’ aliyemsaini mapema mwaka huu, hivyo kufi kisha idadi ya wasanii wake wawili.
Harmo aliweka posti kwenye ukurasa wake wa Instagram akimkaribisha Skales kwenye Lebo ya Konde Gang; “We are happy to welcome genius musician from Nigeria, my brother @youngskales welcome to the family @ kondegang is a dream team.”
Baada ya kutangaza kumsaini Skales kama msanii wake, ndipo utata ukaibuka kufuatia staa huyo wa Nigeria kusema kuwa hajasainiwa kama msanii wa Konde Gang, bali lebo hiyo itahusika kusimamia kazi zake kwa ukanda wa Afrika Mashariki.
“Hello my East African lovers, i have offi cially come on board with Konde Music, the team will now stand as my management in East Africa,’’ aliandika hivyo Skales akimaanisha kuwa yupo kwa ajili ya kusimamiwa kazi zake tu kwa ukanda wa Afrika Mashariki na si kama msanii wa lebo hiyo.
Skales ni mwanamuziki mkubwa ambaye ametoa nyimbo nyingi kali na mojawapo amefanya na Harmo inayokwenda kwa jina la Fire Waist.
STORI: HAPPYNESS MASUNGA, DAR GPL
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake