WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza wakati alipoongoza
harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la
Anglikana Dayosisi ya Tanga Mtaa wa Mtakatifu Augustino wa Hippo
Chumbageni
Tanga kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kushoto ni Canon
Rev Chistopher Kiango ambaye ni Kasisi kiongozi wa Kanisa la Anglikana
Dayosisi ya Tanga
Canon
Rev Chistopher Kiango ambaye ni Kasisi kiongozi wa Kanisa la Anglikana
Dayosisi ya Tanga akizungumza wakati wa harambee hiyo
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa halfa hiyo
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto
akipokea zawadi ya kuku kutoka kwa Katibu wa Kanisa Anglikana Dayosisi
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto
akipokea mchango wa mtoto Nicolaus Galula wakati wa harambee hiyo
MENEJA wa Hotel ya Tanga Beach ya Jijini Tanga Joseph Ngoyo akizungumza jambo wakati wa harambee mara baada ya kukabidhi mchango wake kwa niaba ya familia yake
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto
akipokea mchango kutoka kwa Catherine Kitandula wakati wa harambee hiyo
Kwaya ikitumbuiza wakati wa harambee hiyo
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka viongoziwa dini kote nchini kuendelea kuliombea Taifa amani, umoja na mshikamano kuelekea
uchaguzi mkuu.
Ummy aliyasema hayo leo wakati alipoongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la
Anglikana Dayosisi ya Tanga Mtaa wa Mtakatifu Augustino wa Hippo Chumbageni
Tanga.
Katika harambee hiyo walifanikiwa kukusanya fedha taslimu milioni 13.7 papo hapo na
ahadi ikiwa ni milioni 47.2.huku mwisho wa kukusanya michango hiyo ikiwa ni
Septemba 20 mwaka huu.
Katika harambee hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa na
viongozi wa dini wakiwemo waumini huku kwaya mbalimbali zikitumbuikza
“Lakini pia tunawashukuru viongozi wa dini kwa jinsi walivyotuunga mkono kwa sala za
kila siku katika mapambano dhidi ya Corona na mungu akatuepusha na janga hili
hivyo niwaombe hata wakati huu nchi ikielekea kwenye uchaguzi mkuu tuendelee
kuiombea nchi”Alisema Waziri Ummy
“Nimekuwa nikipata ujumbe kutoka kwa mawaziri wa nchi nyengine Afrika tumefanya kitu gani
mpaka hakuna Corona nisema kwamba ugonjwa huo umetoweka kutokana na Mungu ameipenda Tanzania”.
Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi Katibu wa Kanisa hilo Cyprian Mtweve alisema
lengo la harambee ya leo katika kuadhimisha sikukuu ya Mt.Agustino wa Hippo ni
kupata kiasi cha sh.milioni 125 kwa ajili ya kuezeka kanisa.
Alisema wanaamini kiasi hicho sio kikubwa kwa Mungu cha kushindwa kupatikana huku
wakimshukuru mgeni rasmi kuwaongozea zoezi la harambee hiyo na kushiriki kwa
moyo na kwa ukamilifu.
Aidha alisema upanuzi wa jengo la kanisa hilo umekuwa ukifanywa kwa kulirefusha kwa
kiwango ambacho mawasiliano baina ya kasisi anayeongoza ibada madhabahuni na
waumini wanaokaa viti vya mwishoni nyuma ya kanisa yanakuwa hafifu sababu ya
umbali.
“Jengo hili limejengwa kwa kutumia teknologia ya zamani isiyohimili uwekwaji wa mifumo
mbalimbali ya kisasa ikiwemo ile itakayoboresha ibada”Alisema
Miongoni mwa viongozi ambao wamechangia kwenye harambee hiyo ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
John Kijazi na Profesa Palamagamba Kabudi wakiwemo wakuu wa wilaya .
No comments:
Post a Comment