Monday, September 14, 2020

HALMASHAURI MJI WA GEITA YAELEZEA MIRADI MBALIMBALI WANAYOITEKELEZA

Mchumi wa halmashauri hiyo Emmanuel Magesa akiwaelezea waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali kuhusu ujenzi wa machinjio ya kisasa yanayojengwa katika eneo la Mpomvu kata ya Mtakuja mjini Geita.
Injinia Abdalla Yasin kutoka kampuni ya GIPCO Construction ltd inayojenga mradi huo akitoa maelezo kwa waandishi wa habari waliotembelea mradi huo leo eneo la Mpomvu kata ya Mtakuja mjini Geita.
Dk. Brian Mawala ambaye ni Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita akiwaelezea waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa hospitali hiyo ambayo imekamilika na kuanza kutoa huduma.
Mchumi wa halmashauri hiyo Emmanuel Magesa akiwaelezea waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali kuhusu majengo ya Soko la madini mjini Geita yanayomilikiwa na halmashauri hiyo.
Soko la Wajasiriamali Kitundu mjini Geita.
Jengo la Halmashauri ya wilaya ya Geita linalojengwa katika eneo la Magogo kata ya Bombambili ambako ndiko mji wa serikali unajengwa.
Majengo ya Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita yaliyopo Magogo kata ya Bombambili mjini Geita.

NA JOHN BUKUKU- GEITA

HALMASHAURI ya Mji wa Geita inatekeleza Ujenzi wa miradi mbalimbali katika halmashauri ya hiyo ambapo ujenzi wa miradi inaendelea vizuri huku miradi hiyo ikitarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu .

Kuna miradi kadhaa kama ujenzi wa machinjio ya kisasa inayojengwa eneo la Mpomvu kata ya Mtakuja mjini Geita kwa gaharama ya shilingi Bilioni 7.23 ambayo ujenzi wake umefikia hatua nzuri ili kukamilika

Pia kuna mradi wa Jengo la Halmashauri ya mji wa Geita ambao unaendelea vizuri na unatarajia kukamilika mwishoni mwa mwaka huu na kwamba ujenzi wa jengo hilo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 5.82 na linatarajiwa kupunguza kwa kiwango kikubwa changamoto zinazokabili utendaji kazi wa watumishi wa halmashauri hiyo kutokana na udogo wa jengo linalotumika sasa ambalo chumba kimoja kinachukua watumishi sita.

Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea miradi hiyo na kujionea hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ujenzi huo mchumi wa halmashauri hiyo Emmanuel Magesa amesema jengo hilo linajengwa katika eneo la Magogo kata ya Bombambili ambapo iliamriwa jengo lijengwe eneo hiloambalo limepangwa kuwa mji wa maofisi na idara mbalimbali za Serikali.

Amesema ujenzi wa ilianza mwaka 2017 ambapo Serikali kuu iliipatia halmashauri hiyo kiasi cha shilingi bilioni 1.8 kwa awamu ya lakini halmashauri ikaongeza milion 700 tukatumia Billioni 2.55 ambapo awamu hiyo ilikuwa kujenga na kuezeka na awamu ya pili hivi sasa imefikia aslimia 85.

Magesa amesema jengo hilo litakuwa na ofisi 114 kumbi za mikutano, huduma za kifedha kama mabenki kwa ajili ya ukusanyaji mbalimbali wa mapato ya serikali pamoja na kantini kwa ajili ya watumishi na wageni mbalimbali watakaofika katika jengo hili.

Pia huduma zingine ni pamoja na mifumo mbalimbali ya kifedha pamoja na huduma zingine inayotakiwa kuwekwa kwenye jengo hili tumeshapanga maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuifunga mifumo hiyo.

Magesa ameongeza juzi wamepokea fedha kutoka serikali kuu kiasi cha shilingi milioni 400 ambapo ukamilishajiwa jengo hili unaendelea vizuri ni matarajio yetu kwamba ifikapo mwezi wa 10 mwaka huu tutaanza kuhamia katika jengo hili.

“Tunaamini kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli imetenda kwa vitendo kwa sababu ilikuwa ni ndoto kwamba tunaweza kujenga jengo kubwa kama hili na kumaliza.”

Akizungumzia majengo ya soko la Dhahabu yaliyopo mjini Geita Magesa amesema soko hilo ni la kwanza kuanzishwa hapa Tanzania , Kama halmashauri ya mji wa Geita tumejenga kwa fedha zetu wenyewe.

Amesema soko hilo limegharimu kiasi cha shilingi bilioni 5.8 na toka limejengwa limeleta manufaa na faida kubwa sana kwa halmashauri na serikali kwa ujumla kwa mfano biashara iliyofanyika kwa mwezi wa saba peke yake ni shilingi bilioni moja kwa siku na kuna hii inaifanya halmashauri yetu kukusanya fedha za kutosha na kuongeza pia mapato ya serikali kuu.

“Hapa kuna miundombinu yote inayotakiwa ili kumfanya mfanyabiashara wa madini asihangaike kutafuta soko kuna ofisi zote za serikali zinazohusika na madini kama vile TRA, Kituo cha polisi, Uhamiaji, Mabenki, Ofizi za wanunuzi wa madini wenye leseni, Chumba maalum cha kuchenjua madini ya dhahabu(Smeltig Room) na kadhalika” amesema Magessa.

Amesema maono ya Rais Dk. John Pombe Magufuli yana manufaa makubwa sana kwa nchi hasa kwa upande wa madini yaani mtu mwenye madini ya dhahabu kwa sasa hawezi kuhangaika kutafuta soko badala yake anakuja hapa na kuuza madini yake bila tatizo huku akijipatia fedha yake na serikali ikipata kodi zake zinazostahili kutokana na biashara hiyo..

Pia utoroshaji wa madini umedhibitiwa kwa kiwango kikubwa kwa sababu bei ya dhahabu ya nje na ndani ya nchi zinawekwa hadharani hivyo muuzaji anajua soko lilivyo kwa kila siku na kuna mashine za kupima madini ili kujua kama ni halisi au siyo halisi.

Amesema mradi mwingine ni soko la wafanyabiashara ndogondogo la Kitundu ambalo limejengwa kwa gharama ya shilingi 1.18 na tayari wafanyabiashara wa bidhaa mbalimbali wanaendelea kufanya biashara zao hivyo kuongeza mapato ya halmashauri kupitia tozo mbalimbali.

Mradi mwingine ambao umetembelewa na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari ni hospitali ya rufaa ya mkoa wa Geita ambayo imejengwa kwa gaharama ya shilingi Bilioni

Dk. Brian Mawala ambaye ni Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita amesema awamu ya kwanza ya ujenzi wa hopitali hiyo ilikuwa na jengo la wagonjwa wa nje , Jengo la Ufuaji, Kantini na jengo la ghorofa nne ambalo linachukua vyumba vya upasuaji na (Radiology).

Ameongeza hospitali hiyo imeanza moja kwa moja na huduma zote za kibingwa na baadhi ya upasuaji ili kusaidia jamii iliyokuwa ikipata shida ya kupata huduma mbalimbali zikiwemo za kibingwa.

Hospitali hii ya mkoa ikikamilika ambayo tunatarajia iwe na majengo 13 mpaka 16 ina uwezo wa kuhudumia wagonjwa wa nje 700 hadi 1000 kwa siku na ina uwezo wa kuchukua vitanda visivyopungua 428 ukilinganisha na hospitali yetu ya sasa ambayo ina vitanda 250 kwa hiyo itasaidia sana kupunguza changamoto za kiafya zinazowakabili wananchi

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake