Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Teresia Mtewele akifafanua jambo kwa wananchi wa kata ya Nyalumbu wakati wa kampeni za kuwanadi madiwani na mgombea ubunge wa jimbo la kilolo
Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Teresia Mtewele akifafanua jambo kwa wananchi wa kata ya Nyalumbu wakati wa kampeni za kuwanadi madiwani na mgombea ubunge wa jimbo la kilolo
Na Fredy Mgunda,Kilolo.
Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Teresia Mtewele wananchi wa kata ya Nyalumbu na Ilula jimbo la Kilolo mkoani mkitaka kupata maendeleo kwa haraka chagueni wagombea wanaotokana na chama cha mapinduzi (CCM)
Akizungumza kwenye mkutano wa kuwanadi madiwani na mgombea ubunge wa jimbo hilo, Mtewele alisema kuwa wananchi wanapaswa kuwachagua wagombea wa chama cha mapinduzi kwa kuwa chama hicho ndio kinaweza kuleta maendeleo tofauti na vyama vingine
Alisema kuwa chama cha mapinduzi kimejipanga kuhakikisha kinaleta maendeleo katika kata ya Ilula na Nyalumbu kwa kuwa tayari wamejipanga kwa mikakati imara ya kufanya kazi za kimaendeleo.
Mtewele alisema kuwa anajua kuwa kata ya Ilula na Nyalumbu wanakabiriwa na changamoto ya ukosefu wa huduma za afya kwani hawana kituo cha afya wala zahanati hivyo wakipewa ridhaa ya kuongoza kata hizo watahakikisha wanatafuta ufunzi wa kero hiyo kwa haraka Mtewele
"Najua kina mama wanajua kukiwa na tatizo kiafya hakuna shughuli za kimaendeleo ambazo zitafanyika kwa urahisi hivyo tupeni miaka mitano hiii tuboreshe sekta ya afya kwa kuwa viongozi wa CCM wamejipanga kutatua tatizo hilo"alisema MNEC Mtewele
Mtewele alisema kuwa kata ya Nyalumbu na Ilula zinakabiriwa na tatizo la ukatili wa wa kijinsia na watoto hivyo wakipewa miaka mitano watahakikisha wanakomesha kabisa tatizo na kuwaacha wananchi wakiwa hawana hofu tena na swala hilo la ukatili.
Aidha Mtewele alisema kuwa tatizo la maji limetatuliwa katika kata hizo kutokana kazi kubwa iliyofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufulu.
Alisema kuwa wananchi wa Ilula na Nyalumbu wanategemea kilimo kwa kiasi kubwa hivyo ni lazima kuwasaidia kupandisha thamani ya mazao ili wakulima hao wapate faida ya kilimo hicho.
Mtewele alimazia kwa kuwaomba wananchi wa kata ya Ilula na Nyalumbu kumchagua mgombea udiwani,ubunge na mgombea urais wa CCM kwa kuwa hao ndio wanaweza kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wa kata hizo.
Kwa upande wake mgombea ubunge wa jimbo la Kilolo kupitia chama cha mapinduzi Justine Nyamoga alisema kuwa atakuwa kiongozi wa vitendo na sio maneno kama ilivyokuwa kwa viongozi wengi hivyo wananchi wanapaswa kuchangua kwa kura nyingi ili aweze kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Nyamoga alisema kuwa wananchi wa kata ya Ilula na Nyalumbu wanabiliwa na changamoto ya afya,mikopo ya kibiashara na elimu ya ujasiliamali hivyo akipewa ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha anatatua changamoto hizo.
Aliwaomba wananchi wa kata ya Ilula na Nyalumbu kuhakikisha wanakipigia kura zote kwa wagombea wa chama cha mapinduzi kwa ajili ya maendeleo ya jimbo hilo na kata hizo.
No comments:
Post a Comment