ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 14, 2020

MRADI WA BOMBA LA MAFUTA HOIMA – TANGA KUSHUSHA NEEMA TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea mbele ya mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kutia saini Waraka wa Pamoja Unaoagiza kuanza haraka mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania) kwenye sherehe fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita leo Jumapili Septemba 13, 2020
Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akiongea baada ya kutia saini Waraka wa Pamoja Unaoagiza kuanza haraka mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania) kwenye sherehe fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita leo Jumapili Septemba 13, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakitia saini Waraka wa Pamoja Unaoagiza kuanza haraka mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania) kwenye sherehe fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita leo Jumapili Septemba 13, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakishuhudia mawaziri wa Nishati wa nchi zao ( Mhe. Mary Goretti Kitutu wa Uganda na Dkt. Medard Kalemani wa Tanzania) wakitia saini mkataba wa kuanza haraka mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania) kwenye sherehe fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita leo Jumapili Septemba 13, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akimsindikiza mgeni wake anayeagana na mawaziri wa Tanzania wakati akiondoka kurejea nyumbani baada ya kutia saini Waraka wa Pamoja Unaoagiza kuanza haraka mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania) kwenye sherehe fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita leo Jumapili Septemba 13, 2020

NA JOHN BUKUKU- CHATO -GEITA

Tanzania na Uganda zimekubaliana katika ugawanaji wa faida Tanzania kuchukua asilimia asilimia 60 na Uganda kuchukua asilimia 40 kutokana na bomba la mafuta litakalojengwa kutoka Uganda mpaka Tanzania kupita kwenye eneo kubwa la Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli ameyasema hayo leo kwenye uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita baada ya kutia saini pamoja na mwenzake Rais wa Uganda Mh.Yoweni Museveni katika makubaliano ya waraka wa pamoja wa Makusudio ya utekelezaji wa mradi wa Bomba la Kusafirishia Mafuta Ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda mpaka Tanga Tanzania .

Rais Magufuli amesema kutokana na ugawaji wa faida hiyo Rais Museveni amefanya uamuzi mkubwa kwasababu bomba hilo litapita katika eneo kubwa la Tanzania litakalokuwa na urefu wa kilometa 1,445.

Amesema baada ya kusaini mkataba huo wataalamu wa pande zote mbili wa Uganda na Tanzania wasicheleweshe mradi huo katika vimikataba vidogo vidogo vya makubaliano vilivyobaki .

“Tunataka matokeo na matokeo yawe chanya,katika mkataba huu ambao Rais Museveni amesaini na mimi nimesaini sasa nione wataalamu wa upande wangu atakaechelewesha na najua kwa Mzee Museveni hatakubali wataalamu wake wacheleweshe,tunataka maendeleo ya nchi hizi yawe ya spidi kubwa kwa Tanzania na Waganda,”amesema

Dkt.Magufuli amesema kupitia wataalamu hao wa Uganda waliogundua mafuta hayo ,wataalamu hao watakuja nchini kuangalia mafuta katika Mbuga ya wembere ambapo kunadaiwa tayari kuna mafuta.

Amesema endapo mafuta hayo yatagundulika yataunganishwa katika bomba hilo na kuanza kuuza na kuwa mabilionea.

“Mei 26,2017 nchini mbili zilisaini mkataba wa ushirikiano wa mradi huu,Agosti 5,2017 liliwekwa jiwe la msingi mkoani Tanga na Novemba 9,2017 tukaweka jiwe la msingi pale Lusinga upande wa Uganda ,leo tumetekeleza hatua nyingine muhimu kuelekea utekelezaji wa mradi huu mkubwa,”amesema Dkt. Magufuli.

Uwekaji wa saini wa mkataba huu ni hatua muhimu katika kuelekea kuanza utekelezaji wa mradi huo,ambao ni mkubwa utakaogharimu mabilioni ya fedha.

Dkt.Magufuli amesema takribani dolla za marekani bilioni 3.5 sawa na trilioni 8.8 za Tanzania zitatumika kwa ajili ya mradi huo.

Rais Magufuli ameongeza kuwa Bomba hili ni muhimu kwa ustawi wa uchumi wa nchi zote mbili na nchini Tanzania mradi huu utapita katika mikoa nane,Wilaya 24,Kata 132 na vijiji zaidi ya 136.

“Mradi huu unafaida nyingi kwani bomba hili ni refu zaidi na yatatumika mabomba yanayotumia teknolojia ya kupasha joto duniani,sehemu kubwa ya bomba hilo kilometa 1115 zitakuwa upande wa Tanzania na 330 zitakuwa upande wa Uganda,”amesema

Dkt.Magufuli ameeleza kuwa mikoa ambayo bomba litajengwa ni pamoja na Mkoa wa Kagera,Geita Shinyanga ,Tabora ,Singida,Dodoma,Manyara na Tanga na miongoni mwa wilaya ambazo bomba hilo litapita ni pamoja na Chato,Bukombe na Geita.

“Unaweza kuona ni kwa namna gani mradi huu una umuhimu ,mradi huu umeshughulikiwa kwa muda mrefu,nimpongeze Mzee Museveni amefanya mambo yasiyowezekana kwa Afrika mashariki kuwa na mafuta tulikuwa tukisikia mafuta yapo uarabuni huyu Mzee Museveni ameyatafuta tena kwa kutumia wataalamu wa Uganda ,”amesema

“Tathimini ambayo imefanyika katika kilometa1115 kwa upande wa Tanzania watu watakaoguswa katika maeneo yao ni takribani watu 9000 watalipwa fidia ya bilioni 21 pia wapo watu watakaopitiwa na vituo 14 vitakavyojengwa watu hao nao watalipwa zaidi ya bilioni 9.9,”amesema

“Mradi huo ni mkombozi katika nchi ya Tanzania ,na ni historia nyingine ya pekee na ya ushindi baada ya vita vya kagera tulipomshinda Idd Amin alipokimbilia Uganda ulikuwa ushindi wa kwanza hivyo huu ni ushindi wa pili wa uchumi wa nchi zote mbili.

No comments: