Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Tarifa kwa Wananchi (TCIB), Deus Kibamba akiwasilisha mada kwa Asasi za Kiraia (HAZIPO PICHANI) leo wakati wa semina ya utekelezaji na ufanikishaji wa mikataba wazi kwenye manunuzi ya umma Tanzania iliyofanyika Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wadau wa Asasi za Kiraia wakimfatilia kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Tarifa kwa Wananchi (TCIB), Deus Kibamba(HAYUPO PICHANI) leo wakati wa semina ya utekelezaji na ufanikishaji wa mikataba wazi kwenye manunuzi ya umma Tanzania iliyofanyika Jijini Dodoma.
Wadau wa Asasi za Kiraia wakiwa katika picha ya pamoja baada ya semina ya utekelezaji na ufanikishaji wa mikataba wazi kwenye manunuzi ya umma Tanzania iliyofanyika Jijini Dodoma.
Na. Majid Abdulkarim, Dodoma
Asasi za kiraia nchii zimetakiwa kuwa na uelewa juu ya utekelezaji na ufanikishaji wa mikataba wazi kwenye manunuzi ya umma ili kusaidia wananchi kuhoji pale mikataba iliyoingiwa inaposhindwa kutoa matokeo chanya kwa jamii.
Wito huo umetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Tarifa kwa Wananchi (TCIB), Deus Kibamba leo wakati wa semina ya utekelezaji na ufanikishaji wa mikataba wazi kwenye manunuzi ya umma Tanzania iliyofanyika Jijini Dodoma.
Kibamba amesema kuwa Manunuzi ya serikali yanahitaji kufanyika katika uwazi kuanzia hatua za mwanzoni kabisa kwenye kuandaa mradi, kutangaza tenda ,kutoa tenda kwa wazabuni na hata utekelezaji wa mradi ili wananchi kuwa na uelewa juu ya miradi inayotekelezwa .
“Tanzania inapambana kutatua tatizo hilo ili miradi ikamilike kwa wakati, ufanisi na ubora uendane na thamani ya pesa ya mradi husika”, amesisitiza Kibamba.
Aidha Kibamba amesema kuwa wameandaa kitabu kinachonatoa taarfa mbalimbali zinazohuhusu matumizi mabaya ya mali za umma hasa katika ughavi wa umma, hali ilivyo sasa na pia majukumu ya bunge na taasisi zake katika kushughulikia suala hilo.
Kitabu hicho kinalenga wabunge na jamii kwa ujumla kuwa na uelewa juu ya miradi inayotekelezwa katika maeneo yao hapa nchini ili mikataba na miradi hiyo kuleta matokeo chanya kwa wananchi wamaeneo husika.
“Lengo la kuwa na uelewa wa kitabu hicho ni kuimarisha utawala bora unaojikita katika uwazi , wajibikaji , unaoshirikisha raia katika mambo yake na unaofata sheria”, ameeleza Kibamba.
Kibamba ameongeza kuawa uelewa huo kwa asasi za kiraia utasaidia Kufanikisha taasisi imara katika kutekeleza malengo endelevu ya maendeleo kwa jamii.
No comments:
Post a Comment