Thursday, October 15, 2020

MATUKIO MBALIMBALI YA PICHA WAKATI MGOMBEA URAIS WA CCM DK. JOHN POMBE MAGUFULI ALIPOUNGURUMA TANGANYIKA PARKERS KAWE JIJINI DAR ES SALAAM

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Tanganyika Parker’s Kawe jijini Dar es Salaam leo Jumatano Oktoba 14, 2020.

Rais Dk. Magufuli amewaomba watanzania kuichagua CCM na wagombea wa Chama hicho kwa sababu ndicho chenye uwezo wa kuyaenzi yote mazuri aliyoyaacha baba wa Taifa Mwalimu J. K. Nyerere ikiwa ni pamoja na kulinda amani ya nchi na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao ulizaa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

(PICHA NA JOHN BUKUKU-KAWE)
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Tanganyika Parker’s Kawe jijini Dar es Salaam leo Jumatano Oktoba 14, 2020 kutoka kulia ni Mgombea ubunge wa jimbo la Kawe Askofu Josephat Gwajima, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam mama Kate Kamba na katikati ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dk. Bashiru Ali.
Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dk. Bashiru Ali, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam mama Kate Kamba, Mgombea ubunge wa jimbo la Kawe Askofu Josephat Gwajima na mgombea ubunge jimbo la Kinondoni Ndugu Abbas Tarimba.
Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Rodrick Mpogolo na kushoto ni Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Humphrey Polepole na baadhi ya viongozi wakiwa wameketi jukwaa kuu.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam mama Kate Kamba akizungumza wakati akimkaribisha Rais Dk. John Pombe Magufuli ili kuzungumza na wananchi katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam mama Kate Kamba kulia na Mgombea ubunge wa jimbo la Kawe Askofu Josephat Gwajima wakiwa katika mkutano huo.
Mwanamuziki Ali Kiba akifanya vitu vyake jukwaani.
Picha mbalimbali zikionesha Baadhi ya wagombea udiwani kwa tiketi ya CCM katika jiji la Dar es salaam na viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi CCM wakiserebuka wakati mwanamuziki Ali Kiba alipokuwa akitumbuiza.
Vibe la wananchi wakinyoosha mikono yao juu kuashiria kumuunga mkono mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dk. John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akiwahutubia kwenye viwanja vya Tanganyika Parkers Kawe jijini Dar es salaam.
Mwanamuziki Naseeb Abdul “Diamondplatnamz” pamoja na kundi lake wakiamshaamsha katika mkutano huo mkubwa wa kampeni kwenye uwanja wa Tanganyika Parkers Kawe jijini Dar es salaam.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiondoka mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dk. John Pombe Magufuli kumaliza hotuba yake.
Picha mbalimbali ya picha zikionesha maelfu ya wananchi waliojitokeza kwenye uwanja wa Tanganyika Parkers Kawe jijini Dar es salaam ili kumzikiliza mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Rais Dk. John Pombe Magufuli.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake