Friday, October 16, 2020

NEC Yakabidhi Nakala Ya Daftari La Wapiga Kura Kwa Vyama Vya Siasa

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) leo Oktoba 15, 2020 imekabidhi vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi mkuu nakala tepe ya daftari la kudumu la wapiga kura linahusisha picha, majina na taarifa za wapiga kura.

Pia wamekabidhi Karatasi ya mfano ya kupigia kura yenye orodha ya wagombea nafasi ya urais na makamu wa rais

Kanuni ya 37 ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mwaka 2018 inaelekeza Tume inaweza kuvipatia vyama nakala ya Daftari hilo kwa ajili ya utambuzi wa wapigakura wanaoingia Kituoni.

Masharti ya kanuni ya 50 (1) ya uchaguzi wa Rais na wabunge ya mwaka 2020, wasimamizi wa uchaguzi watavipatia vyama vya siasa orodha ya vituo vya kupigia kura ili vyama vipange mawakala.

Pia NEC imetangaza vituo 80,155 vya wapiga kura kwa Tanzania bara

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake