MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, amekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni zikidai kuwa kwamba polisi imewapiga risasi na kuwaua watu watatu Visiwani Pemba katika tukio la jana usiku.
Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es-Salaam asubuhi ya leo, amesema Jeshi la Polisi linawashikilia vijana 42 mpaka sasa visiwani Zanzibar kutokana na vurugu za jana usiku zilizotokea Pemba wakati wa kusambaza vifaa vya kupigia kura.
Chama cha ACT Wazalendo kimedai kuwa watu wanne wameuaa katika vurugu hizo huku wengine wakijeruhiwa.
IGP Sirro amefafanua kuwa vijana waliokamatwa walikuwa wanawarushia mawe polisi na baadhi ya maafisa wa uchaguzi waliokuwa wanasambaza masanduku ya kupiga kura eneo hilo kabla ya uchaguzi wa mapema unaoendelea hii leo.
Aidha, ameonya kuwa mtu au watu waliopanga kusalia kwenye vituo vya kupigia kura baada ya kupiga kura zao kwa madai kwamba wanalinda kura akisema hilo halikubaliki na haliwezi kuvumiliwa. Pia amewataka wananchi kuwa na utulivu na kudumisha amani katika kipindi hiki cha uchaguzi.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake