Sunday, October 4, 2020

TAMISEMI YAJIVUNIA MSAADA WA CAMFED KWA WANAFUNZI TANZANIA

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare (wa pili kulia) akimkabidhi cheti mmoja wa waongozaji wa program ya ‘Dunia Yangu Bora’ kwenye hafla hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya CAMFED, Bi. Jeanne Ndyetabura akishuhudia.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare (wa pili kulia) akimkabidhi cheti mmoja wa waongozaji wa program ya ‘Dunia Yangu Bora’ kwenye hafla hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya CAMFED, Bi. Jeanne Ndyetabura akishuhudia.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare, akizungumza akimwakilisha mgeni rasmi, Waziri wa TAMISEMI, Mh. Selemani Jafo kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya CAMFED, Bi. Jeanne Ndyetabura akizungumzia kuhusu ushirikiano uliopo kati ya CAMFED na serikali katika kufanya kazi na kuwezesha wasichana. 
Mkurugenzi wa CAMFED, Bi. Lydia Wilbard akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika mkoani Morogoro.
Mkurugenzi wa Elimu toka TAMISEMI, Bw. Julius Nestory akielezea kwanini Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imeona umuhimu wakutambua mchango wa waongozaji wa program ya ‘Dunia Yangu Bora’. kwenye hafla hiyo.
Na Mwandishi Wetu, Morogoro

SERIKARI kupitia TAMISEMI imesema inajivunia na kutambua msaada mkubwa unaotolewa na Shirika la CAMFED kwa wanafunzi wasichana na wana jamii na waongozaji wa wanafunzi shuleni lengo likiwa ni kuwezesha na kuwainua kiuchumi. 

Kauli imetolewa na Waziri wa TAMISEMI, Mh. Selemani Jafo kupitia hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Loata Ole Sanare katika hafla ya kuwatunuku vyeti waongozaji wa wanafunzi waliochini ya program za Shirika la CAMFED iliyofanyika mkoani Morogoro.

Katika hotuba hiyo ya Waziri Jafo aliyekuwa mgeni rasmi, alisema TAMISEMI, inajivunia na kutambua msaada unaotolewa kwa wanafunzi na kwa jamii na waongozaji wa wanafunzi katika programu mbalimbali za CAMFED kuanzia mashuleni na kuwaomba waendelee kuisaidia jamii.

“…Kwa niaba ya Serikali tunapendekeza muendelee kufanya kazi hii nzuri kwani juhudi na dhamira zenu zinapongezwa sana. Kupitia wasichana kama nyinyi, ambao mnasaidia raia wenzenu, taifa letu litaweza kufikia Maono ya Maendeleo ya mwaka 2025, ambayo yanaelezea taifa la raia ambao wana mawazo chanya, na tamaduni ambazo zinachochea maendeleo ya binadamu kupitia kufanya kazi kwa bidii, weledi ujasiriamali, ubunifu, ugunduzi na werevu.


Stumai Kaguna, Mfadhiliwa wa CAMFED na mmoja kati ya waongozaji wa program ya “Dunia Yangu Bora” akielezea jinsi gani program hii ya stadi za maisha imeweza kumsaidia yeye binafsi kutoka katika dimbwi la umasikini na pia ameweza kuwasiaida wanafunzi kujifunza na kuhamasisha vikundi vya wazazi kuchangia maendeleo shuleni ikiwemo chakula.

“Ninashawishika kusema kuwa program hii inastahili msaada wa serikali, na tunafanyakazi pamoja ili kuona ni kwa namna gani inaweza kuwafikia wanafunzi wengi Zaidi katika shule zote nchini.” Alisema Waziri Jafo katika hotuba hiyo.

Akizungumza awali katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa CAMFED, Bi. Lydia Wilbard alisema tangu kuanzishwa kwa CAMFED Tanzania, tayari imewasaidia zaidi ya watoto 683,439 kuhudhuria na kufanikisha masomo yao shuleni, kwa kuzingatia wasichana walio katika mazingira magumu.

Aidha aliongeza kuwa Wanawake vijana 26,376 ambao wamehitimu masomo yao ya sekondari kwa ufadhili wa CAMFED wamenufaika pia baada ya kujiunga katika mtandao wa wafadhiliwa wa CAMFED.

“…CAMFED inatoa mafunzo ya uongozi na ujasiriamali na program za kujitolea. Motisha hizi zinawasaidia kutengeneza ujuzi na maarifa ambao unawawezesha kuboresha fursa za baadaye, pamoja na familia na jamii zao. CAMFED Tanzania inashirikiana pamoja na shule za serikali 819 katika wilaya 32 ndani ya mikoa 9 nchini,” alibainisha Bi. Lydia Wilbard.

Hata hivyo, aliwashukuru wadau wa maendeleo Selikari ya Uingereza (DFID/FCDO) na Taasisi ya ELMA kwa ushirikiano na kuwezesha program ya ‘Dunia Yangua Bora’ na kujitolea kusaidia wasichana waishio katika mazingira magumu kupata elimu, kutoka shule za msingi kwenda sekondari, na kutoka sekondari kwenda katika elimu ya juu, ujasiriamali na ajira.

Hafla hiyo imejumuisha wanawake vijana ambao wamehitimu elimu yao ya sekondari chini ya ufadhili wa CAMFED, na kuamua kujitolea katika shule zao za awali, ambapo wanatoa program ya stadi za maisha inayoitwa “Dunia Yangu Bora” ambayo inakamilisha mafunzo ya kitaaluma ya watoto. “Dunia Yangu Bora” ni programu inayojenga ujuzi kama vile kujiamini,mawasiliano fasaha na kutatua – matatizo, ambayo ni msingi wa ajira zote (rasmi na ajira binafsi).

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake