Saturday, October 10, 2020

WATAALAMU WA TEHAMA WATAKIWA KUJISAJILI ILI WAWEZE KUFAHAMIKA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt.Zainabu Chaula akizungumza katika kufunga Kongamano la Nne la Mwaka la Tehama lililofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es SalaamKatibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt.Zainabu Chaula akipata picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa sekta ya mawasiliano baada ya kufunga Kongamano la Nne la Mwaka la Tehama lililofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam

NA EMMANUEL MBATILO

Wataalamu wa Tehama nchini wamehimizwa kujisajili ili waweze kutambulika na kunufaika na mpango wa mzima wa Serikali wa kuwajengea uwezo.

Ameyasema hayo leo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt.Zainabu Chaula akifunga Kongamano la Nne la mwaka la Tehama kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Akizingumza katika Kongamano hilo Dkt.Chaula amesema kuwa ili serikali ipate wapi pa kuanzia wataalamu wote wanatakiwa kujisajili kwasababu Serikali ishafungua milango ya kufanya hivyo na kitachofuata ni mipango ya kuwaendeleza.

Aidha Dkt.Chaula amesema maonesho hayo yametoa wigo mpana zaidi kwa Watanzania kuweza kuona ni jinsi gani wanaweza kutumia Tehama kujiendeleza kiuchumi.

Pamoja na hayo ameiagiza tume ya Tehama kuanza maandalizi ya Kongamano la lijalo kwa kushirikisha wadau na wajasiliamali.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tehama Bw.Samson Mwela amesema Katika siku hizo za kongamano wameona aina mbalimbali za ujuzi na ubunifu wa mapinduzi ya viwanda hivyo nchi yetu inahitaji kuwajenga wataalamu wao.

“Tumeona ubunifu kwa vijana wetu wa Kitanzania wametengeneza kwaajili ya Shule, Kilimo na huduma mbalimbali za kifedha kwa kuwafikia watu mbalombali”. Amesema Bw.Mwela.

Nae Mhadhili Chuo cha DIT,Bw.Nkundwe Mwasaga amesema Kuwa Katika kongamano Hilo wameweza kujadili Mambo mbalimbali ikiwemo uchumi wa kidijitali kwa maana ndiyo eneo pekee ambalo litabadilisha Mambo mengi ikiwa ni kuleta uchumi wa watu.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake